Polisi wamkamata mwandishi Dar

Polisi wamkamata mwandishi Dar

Halisi

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2007
Posts
2,802
Reaction score
614
Polisi Dar es Salaam leo wamemkamata mwandishi wa habari Moshi Lusonzo, ambaye alikuwa akipiga picha wakati wa operesheni ya polisi ya kukamata wafanyabiashara wanaoiba haki za wasanii katika maeneo ya Kariakoo. Polisi hao wamemnyang'anya mpiga picha huyo kamera yake na kitambulisho wakidai kwamba wameingiliwa katika kazi zao za upelelezi.

Kabla ya operesheni hiyo, polisi hao walipiga simu jana na kutaka waandishi washuhudie jinsi polisi wanavyotekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete katika kukabiliana na wafanyabiashara wanaoiba kazi za wasanii.

Hadi sasa mwandishi huyo yuko kituo cha polisi cha Msimbazi.
 
Kabla ya operesheni hiyo, polisi hao walipiga simu jana na kutaka waandishi washuhudie jinsi polisi wanavyotekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete katika kukabiliana na wafanyabiashara wanaoiba kazi za wasanii
POLICE WA NNCHI HII NI WAJINGA KATIKA MBINU, WANAFANYA KAZI KAMA WANASIASA, KULIKUA NA HAJA GANI KUITA WAANDISHI WA HABARI WAKIWA KAZINI...SIFA ZA KIJINGA, HAWAFANYI KAZI BALI MPAKA RAIS ASEME, KWA HIYO KAMA RAIS ASINGESEMA LISSINGEKUWA KOSA KISHERIA...SHAME ON U kOVA,
 
Kwani ukipigwa picha unafanya kazi tatizo liko wapi? mbona wakiwa wanacheza magwaride wanawaalika waandishi wa habari? wanaopenda vificho wana yao mambo ambayo wooote twayajua
 
Polisi wanafanya kazi kama ROBBOTS!...Never rational!
 
Polisi wetu wanazidi kudhihirisha jinsi wasivyotumia akili katika utendaji wao wa kazi, nguvu kibao lakini vichwani hakuna kitu.
 
alafu hili swala la kutangaza kua kesho tutafanya jambo fulani kwenye vyombo vya habari sijui ndio utendaji gani kwa jeshi la polisi, maana mantiki zima ya kufanya msako ni kukamata, sasa ukitangza jambo sinikwamba unawaambia watu wajifiche...!!! kuna siku hawa polisi walikuawanataka kufanya msako wa kukamata wala bange, vibaka na wazurulaji pale bonde la jangwani, kwa mshangao wangu kamanda kova akawa anatangaza kwenye tv anaongelea juu ya msako huo, nilishindwa kuelewa kabisa nia na dhumuni lake/
 
Mimi nahisi kuna picha ambayo walipigwa wakipokea chochote, wakaona ili kpoteza ushaidi, basi wamkamate huyo mwandishi na kumnyang'anya kamera ili wafute hizo picha
 
Sasa kwanini kama wao wanafanya kazi ya usalama wanyanganye camera za mwandishi wa habari bila la kosa lolote lile
 
Katika lile sakata lililomuweka ndani Mke wa Dr.Slaa , sasa limechukua sura mpya baada ya Polisi Mkoani Arusha kuwakamata waandishi waandamizi wa vyombo mbalimbali vya habari wakati wanafuatilia sakata hilo.

Waandishi waliokamatwa ni;
1. Musa Juma -Mwananchi
2.Elia Mbonea- Rai/Mtanzania
3.Asiraji Mvungi + Mpiga picha wake wa ITV.

Wengine bado majina hayajanifikia ila yakifika ntawahabarisha.

Mpaka sasa wapo ndani na wamenyanganywa vitendea kazi vyao na hata simu na hivyo hawapatikani mpaka sasa.

Walikuwa wanafuatilia hali tete ambayo imejitokeza baada ya wananchi wa Hanang kuamua kuchukua silaha za jadi na haswa mishale ili kupambana na polisi katika kulinda ardhi yao .

FFU wamemwagwa wengi sana kwani mkuu wa wilaya yupo kwa ajili ya kugawa eneo hilo kwa nguvu.

Ntaendelea kuwajuza.
 
2010 - kuna kazi!

Amani na Utulivu na Utengemano upo kwenye "EDGE"!
 
Maumivu ya kichwa huanza pole pole na ni mtu mwenyewe anayasikia wengine wanahadithiwa.

Asante kwa taarifa mkuu
 
FFU wamemwagwa wengi sana kwani mkuu wa wilaya yupo kwa ajili ya kugawa eneo hilo kwa nguvu.

Ntaendelea kuwajuza.

Mamlaka ya Kugawa ardhi anayapata wapi?

Hivi Tanzania leo hii pana Mtanzania hata mmoja anayegawiwa ardhi na serikali?
 
Mamlaka ya Kugawa ardhi anayapata wapi?

Hivi Tanzania leo hii pana Mtanzania hata mmoja anayegawiwa ardhi na serikali?

Mgogoro uliopo ni kati ya wakulima na wafugaji kwani eneo lilikuwa linamilikiwa NAFCO na baada ya NAFCO kufilisika likawa linatumiwa na wakulima ,ila sasa wanataka wafugaji wagawiwe pia eneo hilo ambalo ni maarufu kwa kuzalisha mpunga.

Mkuu wa Wilaya ndio mwenyekiti wa kinachoitwa kamati ya ulinzi na usalama na kiutendaji unakuta kuwa polisi wako chini yake na anaweza kuwaamrisha polisi .
 
Kiranja,

How did NAFCO get all that land in the first place?

Mlenge
 
"Publish or Perish" -- Dunia ya kwanza

"Publish and Perish" -- Dunia ya tatu

-- source: unknown
 
Ndiyo sababu maranyingi Polisi hawapatani na Waandishi wa habari kwa kuhisi na kuzani mambo yao yaandikwa.
Suala la kugawa Ardhi ni lazima Maandishi wawepo kwa ajili ya kuwahabarisha Wananchi.
Kukamatwa kwao sio sasa.
 
Back
Top Bottom