Polisi wamkamata mwandishi Dar

dawa ya FFU ni mabomu ya chumvi....haya hawajui madhara yake.
 
Inaonekana Polisi wanakazi moja na Waandishi wa habari, Kwanza walianza na J. Muro na sasa wanaendelea na wengine, Hii inaonekana ni Kampeni ya kudumu.
Arusha pia Waandishi wa habari wamekamatwa.
 
Sijui hawa polisi wanatoa wapi jeuri ya kuwakamata na kuwanyanganya waandishi wa habari vitendea kazi vyao. Je wao wangenyangwanywa silaa wangechukua hatua gani?
Kama mambo yameanza kuwa hivi, kipindi cha kampeni na uchaguzi wao chonjo, vinginevyo makubwa yatawapata.
 
Poleni sana ndugu zetu Waandishi mliokamatwa. I am pretty sure that this will not the move. Watawakamata na hata kuwatesa lakini wakati wote msimame katika haki. Hii tu ni mojawapo ya ubabe wa serikali ya CCM kwa wananchi wake. Je, si mambo kama haya ndiyo yaliyopelekea watu kuuana Kenya mwaka 2007 (ardhi???). Kwanini serikali igawe ardhi ya wananchi bila ridhaa yao??? Hao wanaoitwa wawekezaji kwanini wasigawiwe mapori wayafyeke wapate mashamba na wananchi wakaachiwa mashamba haya yaliyopo katika maeneo yao??? Hawa wawekezaji wanapewa kila kitu bureee?? waon wanakuja hata bila mitaji kuja kuvuna tuuuu!!! Wapewe mapori tuone mifano ya matumizi ya hiyo mitaji yao ya uwekezaji, hata sisi wananchi tutawasafishia wakitulipa lakini ardhi ilyokwisha safishwa ibaki kuwa ya Watanzania maskini waishio katika maeneo hayo au hawa wawekezaji wakodishe hayo mashamba kutoka kwa wananchi lakini si kunyang'anywa!! Tunahitaji akina Saeed Kubenea wajuze mambo kama haya ya dhuluma pia!!!
 
Siku hizi Hanang haipo Arusha, ipo Manyara - kilometa chache kutoka Babati, Makao Makuu ya mkoa huo!
 
Jamani anayefahamu sheria ambayo polisi wanatumia kumkamata raia na kumuweka ndani na ni katika muda gani ni lazima afikishwe mahakamani? Lingine ni hili la kukamata watu Ijumaa wakijua kwamba mahakama zimefungwa hadi Jumatatu, bila kusahau Je, inawezekana kuomba urgent application mahakamani ili kesi kama hizi zinazoangukia weekend zisikilizwe Jumamosi au Jumapili au siku yoyote isiyokuwa ya kazi? Process ikoje?

Jingine je, huyu polisi ni lazima awe katika mavazi ya kipolisi au anatakiwa kuwa na ushahidi gani kufanya arrest au ni bora awe polisi tu?
 

Kaka kila laheri na ufuatiliaji wako, angalia wasije wakakuchukua na wewe.
 
Kilichonifurahisha zaidi ni kuwa hawa ndugu wamefunguliwa mashitaka ya;
1. Kufanya mkutano bila kibali- eti kwa vile walikuwa wamekusanyika na wananchi na walikuwa wanawahoji hivyo kundi hilo likaitwa mkutano wa hadhara.
2. walikutwa kwenye eneo lenye mgogoro - eti bila kibali sasa sijui nani anatakiwa kuwapa kibali hicho.

Taarifa nilizopata ni kuwa jana jioni walipelekwa Babati na walikutana na Kaimu RCO sasa kilichojiri sijakijua bado.

Kiranja tupatie yaliyojiri huko.
 
Huo haukuwa msako rasmi uliopangwa na makao makuu bali ilikuwa njaa zao wakaamua wafanye kazi hiyo kwa vile hata Rais alikwishatangaza.kwa hiyo hawakuhitaji wanahabari huyo aliyewafumania kawaharibia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…