Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Poleni sana ndugu zetu Waandishi mliokamatwa. I am pretty sure that this will not the move. Watawakamata na hata kuwatesa lakini wakati wote msimame katika haki. Hii tu ni mojawapo ya ubabe wa serikali ya CCM kwa wananchi wake. Je, si mambo kama haya ndiyo yaliyopelekea watu kuuana Kenya mwaka 2007 (ardhi???). Kwanini serikali igawe ardhi ya wananchi bila ridhaa yao??? Hao wanaoitwa wawekezaji kwanini wasigawiwe mapori wayafyeke wapate mashamba na wananchi wakaachiwa mashamba haya yaliyopo katika maeneo yao??? Hawa wawekezaji wanapewa kila kitu bureee?? waon wanakuja hata bila mitaji kuja kuvuna tuuuu!!! Wapewe mapori tuone mifano ya matumizi ya hiyo mitaji yao ya uwekezaji, hata sisi wananchi tutawasafishia wakitulipa lakini ardhi ilyokwisha safishwa ibaki kuwa ya Watanzania maskini waishio katika maeneo hayo au hawa wawekezaji wakodishe hayo mashamba kutoka kwa wananchi lakini si kunyang'anywa!! Tunahitaji akina Saeed Kubenea wajuze mambo kama haya ya dhuluma pia!!!Katika lile sakata lililomuweka ndani Mke wa Dr.Slaa , sasa limechukua sura mpya baada ya Polisi Mkoani Arusha kuwakamata waandishi waandamizi wa vyombo mbalimbali vya habari wakati wanafuatilia sakata hilo.
Waandishi waliokamatwa ni;
1. Musa Juma -Mwananchi
2.Elia Mbonea- Rai/Mtanzania
3.Asiraji Mvungi + Mpiga picha wake wa ITV.
Wengine bado majina hayajanifikia ila yakifika ntawahabarisha.
Mpaka sasa wapo ndani na wamenyanganywa vitendea kazi vyao na hata simu na hivyo hawapatikani mpaka sasa.
Walikuwa wanafuatilia hali tete ambayo imejitokeza baada ya wananchi wa Hanang kuamua kuchukua silaha za jadi na haswa mishale ili kupambana na polisi katika kulinda ardhi yao .
FFU wamemwagwa wengi sana kwani mkuu wa wilaya yupo kwa ajili ya kugawa eneo hilo kwa nguvu.
Ntaendelea kuwajuza.
Katika lile sakata lililomuweka ndani Mke wa Dr.Slaa , sasa limechukua sura mpya baada ya Polisi Mkoani Arusha kuwakamata waandishi waandamizi wa vyombo mbalimbali vya habari wakati wanafuatilia sakata hilo.