Polisi wamsafirisha Niffer hadi Dar kutokea Dodoma baada ya kujisalimisha kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kukamatwa

Polisi wamsafirisha Niffer hadi Dar kutokea Dodoma baada ya kujisalimisha kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kukamatwa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Jeshi la Polisi limemsafirisha kwenda jijini Dar es Salaam mfanyabiashara wa mtandaoni, Jenifer Jovin maarufu Niffer baada ya kujisalimisha polisi jana.

Mfanyabiashara huyo alijisalimisha kwa Jeshi la Polisi jana baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuagiza Jeshi hilo kumhoji kwa kosa la kukusanya fedha za michango kwa ajili ya waathirika walioporomokewa na ghorofa Kariakoo jijini Dar es Salaam bila kibali.
1732001796634.png
Pia, Soma:

Jengo hilo liliporomoka Jumamosi Novemba 16, 2024 na kusababisha vifo vya watu 16, majeruhi 86 na uharibifu wa mali za mamilioni ya fedha.

Akizungumza leo Jumanne Novemba 19, 2024 jijini Dodoma, Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Anania Amo amesema Niffer amekamatwa na polisi baada ya kujisalimisha jana.

“Alijisalimisha jana baada ya kumtafuta, tayari tumemsafirisha kwenda jijini Dar es Salaam,”amesema.

Credit: Mwananchi
 
Hii ni Kiki kwa utawala wamechemka sana.. Tabu hawajui wanaharibu sana kwa wananchi.

Na aliyeshupalia anafurahia sana na gesi. Huku yeye wa Maziwa ya mtoto tangu akue.

Upande wa Niffer ni jambo zuri, litapita hili.
 
NI mateso tosha ya kisaikolojia, i hope ile Strong army iliyo nyuma yake itapata la kujifunza na yeye atajifunza kitu.

Kujifunza nini!!! Kosa limefanyika wange muelimisha wamuachie. Jeshi lipo na serikalini ndio inajichemsha zaidi na zaidi.

Nyota Nyota anayo Niffer.

Atayavuka haya, pesa si wachukue tu haraka wakazile sio kumsumbua mtoto wa watu.
 
Back
Top Bottom