Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Jeshi la Polisi Mkoa Lindi, limemuachia Kiongozi mstaafu wa Chama cha ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe baada ya kumkamata kwa muda kwa tuhuma za kutoa taarifa za vitisho katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika Tunduru mkoani Ruvuma.
Usiku wa kuamkia leo Jumatatu Julai 14, 2025 polisi takribani watano walimkamata Zitto katika hoteli aliyofikia Wilaya Lindi.
Soma Pia: Zitto ashikiliwa na Polisi usiku wa manane Lindi
Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Julai 14, 2025 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, John Imori amesema Zitto alikamatwa kutokana na hotuba yake ya Tunduru aliyotamka, “polisi yeyote atakayebeba kura bandia mwaka huu kama si yeye, mke wake au mtoto wake tutamalizana naye."