Polisi wana nia gani kukata rufaa dhidi ya dhamana ya Lissu?

Polisi wana nia gani kukata rufaa dhidi ya dhamana ya Lissu?

mpk

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
3,115
Reaction score
3,864
Kesi ya Lissu itaigia kwenye historia kwa polisi kwenda mahakama kuu kupinga dhamana ya mtu aliyeshitakiwa na jamuhuri. Kwa mjibu wa Uhuru la jana na Tanzania Daima la leo polisi wanajiandaa kurudi mahakamani kesho kupinga dhamana iliyotolewa na mahakama ya Kisutu.

Hapa napata maswali kadhaa:-

Hivi iliwahi kutokea polisi kukata rufaa ya dhamana ya mtuhumiwa yoyote?

Kama hapana kwa nini itokee kwa Lissu?

Ni kwa nia nzuri? Au baada ya kuzomewa kila sehemu baada ya kuaibishwa na nguri wa sheria Tanzania?

Wana uhakika gani kama hawaangukii pua na kupata aibu zaidi? Kama hoja yao kuu ilikuwa kwamba akiachiwa kwa dhamana atafanya kosa lingine kama hilo na mpaka sasa hajalifanya sasa wataenda na hoja ipi?
 
Hoja yako ni nini hasa?
Kwamba polisi hawana haki ya kukata rufaa au Ni ajabu tu kwa polisi kukata rufaa?
 
~ be first to reply.

Polisi wameamua kufanya siasa mahakamani kwa hoja uchwar.a, wamekua watabiri pia...
 
Hoja yako ni nini hasa?
Kwamba polisi hawana haki ya kukata rufaa au Ni ajabu tu kwa polisi kukata rufaa?
Kukata rufaa kupinga dhamana, nipe kesi moja tu ambayo polisi walishakata rufaa kupinga dhamana
 
Kukata rufaa kupinga dhamana, nipe kesi moja tu ambayo polisi walishakata rufaa kupinga dhamana
Nipe kesi moja tu ambapo mtu alimwita Rais Dikteta Uchwara
 
jingalao kweli wewe UVCCM mmeishiwa sela mmebaki kuandika pumba tu.

swissme
Bavicha ndio wanatafuta kiki ya nitoke vipi...yaani wanaiga style ya Cuf miaka ya tisini
 
Kesi ya Lissu itaigia kwenye historia kwa polisi kwenda mahakama kuu kupinga dhamana ya mtu aliyeshitakiwa na jamuhuri. Kwa mjibu wa Uhuru la jana na Tanzania Daima la leo polisi wanajiandaa kurudi mahakamani kesho kupinga dhamana iliyotolewa na mahakama ya Kisutu.

Hapa napata maswali kadhaa:-

Hivi iliwahi kutokea polisi kukata rufaa ya dhamana ya mtuhumiwa yoyote?

Kama hapana kwa nini itokee kwa Lissu?

Ni kwa nia nzuri? Au baada ya kuzomewa kila sehemu baada ya kuaibishwa na nguri wa sheria Tanzania?

Wana uhakika gani kama hawaangukii pua na kupata aibu zaidi? Kama hoja yao kuu ilikuwa kwamba akiachiwa kwa dhamana atafanya kosa lingine kama hilo na mpaka sasa hajalifanya sasa wataenda na hoja ipi?
Hii itakuwa tom and jerry cartoon toleo jipya
 
Mtoa mada unakusudia kusema nin....hoja yako hasa ni nin.nmesoma mara mbili mbili bado cjakuelewa.ila nmegundua unatatizo la elimu kichwan mwako na sheria hujui
 
Nipe kesi moja tu ambapo mtu alimwita Rais Dikteta Uchwara

Hakuna kesi kama hii kwa sababu kuitwa dikteta uchwara siyo tusi na halijawahi kuwa kosa popote. Sasa unataka kesi itoke wapi? Subiri ya Lisu ndiyo itakuwa ya kwanza duniani.
 
" Watanzania wataona mengi katika utawala huu 2015- 2020. "

By Robert Mugabe.
 
Maamuzi kutoka juu. Unajua polisi wanataka Lissu akae ndani maana anaweza kutoa kauli nyingne alafu waambiwe akamatwe. Sasa polisi nao inaonekana wamechoka kumkamata mtu mmoja kila mara. Sasa wanaona bora akae ndani ili nao wasisumbuke.
 
Back
Top Bottom