Polisi wana wajibu wa kulinda Usalama wa Raia na Mali zao. Hili suala la Wananchi kuwalipa Sungusungu kuwalinda lipoje kikanuni?

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Habari Wakuu,

Kumekuwa na taratibu ya mitaa mbalimbali hasa uswahilini viongozi wanaweka utaratibu wa kuweka Sungusungu kwa ajili ya kuimarisha ulinzi kwa utaratibu wa kila nyumba kuchagia kuwalipa mwisho wa mwezi.

Kukiwa kama nyumba ina wapangaji kadhaabasi kila mpangaji atapaswa kuchangia kiasi kwa ajili ya sungusungu.

Licha ya raia kulazimishwa kwa nguvu na changamoto za sungusungu naomba kujuzwa utaratibu wa mambo machache.

Sungusungu wanaruhusiwa kikanuni?

Kama wanaruhusiwa, ni nani anapaswa kuwalipa? kwa taratibu gani

Kama hawaruhusiwi Wananchi wanapaswa kutoa taarifa kwa nani? Au wafanye nini kuondokana na adha hii?

Nawasilisha
 
Jiunge nao ukapigwe baridi la usiku, buku buku tunazochanga zinawasaidia kupata battery na chochote kitu kusogeza usiku kupita
 
Mbezi Louis Sungusungu wanatishia kuwadhuru watu wanaogoma kuchangia pesa.

Serikali ondoeni huu uchafu unaoitwa Sungusungu.

Watu tunalipa kodi ya mapato Tsh500,000/= kwa mwezi kwanini tugongewe mageti ili tuchangie Sungusungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…