Polisi Wanachangia Uhalifu

Tanzania 1

Senior Member
Joined
Oct 4, 2007
Posts
197
Reaction score
25
Matapeli wengi wamekuwa "wakiwazukia" wananchi kwa kudai kuwa ni askari kanzu na kuwa wana mashaka na mtu/watu "waliowazukia". Lengo lao hasa ni kumtia mshikemshike "mtuhumiwa" wao ili waweze kumchomoa pesa kwa madai ya kuizima "tuhuma" kwa kutoifikisha mbele.

Hili limekuwepo miaka nenda, miaka rudi. Swali: Kwanini Polisi hawatoi tamko la kuwaasa wananchi kutokubali kuhojiwa na yeyote anayedai kuwa ni askari kabla ya "askari" huyo kuonesha kitambulisho?

Wadau wanasheria nakuombeni mtuelimishe zaidi khs sheria za Tz zinazohusiana na suala hili.
 
Siwatetei polisi, najua kuwa wakati mwingine huwa wanawatishia wananchi, na wanawabana wananchi wawape hongo. Ninachotaka kusema ni kuwa hawa polisi wana mishahara isiyoridhisa na general working condition zao siyo nzuri. Tujiulize kwa nini tumewapa madaraka makubwa watu ambao wana kipato kidogo? Lazima tu watayatumia vibaya madaraka yao.

Of course mabosi wao wanapenda rushwa kwa sababu ya uroho wa pesa tu.

Pamoja na kukemea tabia zao zisizoridhisha mapato yao na hali ya kufanya kazi kwao kuangaliwe, vinginevyo tutalea jeshi lapolisi lenye hasira na wananch.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…