Polisi wanne wasimamishwa kazi Kenya

Polisi wanne wasimamishwa kazi Kenya

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Hatimaye serikali ya Kenya imeonekana kuchukua hatua dhidi ya mauaji na ukatili unaoripotiwa kuendelezwa na maafisa wa polisi wanapoidhinisha amri ya kutotoka nje ya saa moja usiku hadi saa kumi na moja asubuhi.
Idara ya usalama imetangaza kuwa polisi wanne wamesimamishwa kazi kusubiri uchunguzi. Haya yanajiri huku watu wawili zaidi wakiripotiwa kuwaua katika maeneo ya Kakamega na Kwale.

Marcus Ocholla, kamanda wa polisi mkoani bonde la ufa amethibitisha kupokea ripoti kadhaa kuhusu maafisa wa polisi kuwajeruhi raia.

Katika muda wa wiki moja sasa, kumekuwa na ongezeko la matukio ya maafisa wa polisi kutumia nguvu kupita kiasi kukabiliana na wakenya wanaopatikana nje baada ya kuanza kwa muda wa marufuku ya kutembea usiku.

Hapo jana watu wawili zaidi waliripotiwa kuwaua huko Kakamega na Kwale.

Watu 10 wanauguza majeraha na wengine wamelazwa hospitali kufuatia ukatili wa polisi
Mjini Busia zaidi ya watu 10 wanauguza majeraha, wengine wakiwa wamelazwa hospitalini baada ya polisi kuingia kwa nguvu katika boma moja walimokuwa wamejifungia baada ya masaa ya kutembea kuisha. Benard Orenga mmoja wa waathirika anakana kwamba hilo si eneo la burudani.

Kamanda wa polosi Ocholla ameeleza kuwa tayari wamechukua hatua kama serikali, ya kuwasimamisha kazi maafisa wanne wa polisi, huku wakuu wawili wakipewa uhamisho.

Kesi iliyowasilishwa na Chama cha mawakili nchini kenya, LSK, kupinga uhalali wa amri ya kutotembea usiku iliyotangazwa na serikali itasikilizwa tarehe 9 mwezi huu.

Hata hivyo, katika uamuzi wa awali polisi wameagizwa kutotumia nguvu katika kuidhinisha amri ya kafyu.

Chanzo: DW
 
Hivi wale police waliohusika na Akwelina huku bongo waliishia wapi?
 
Back
Top Bottom