Polisi wapunguze presha ili wasiwape wahalifu nguvu.

Polisi wapunguze presha ili wasiwape wahalifu nguvu.

robbyr

Senior Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
129
Reaction score
221
Nalipongeza jeshi la polisi kwa kazi nzuri ambayo wameendelea kufanya kwenye taifa hili.
Ila lengo la andiko hili ni kusema kuwa polisi wanapresha ambayo inasababishwa na wao kutuhumiwa katika maswala utekaji.

Rai yangu ni kwa polisi kuwa na utulivu katika utoaji wa taarifa ili kuepusha taharuki nasi kutoa taarifa ili waonekane wanawabijika ambapo baadae zinaleta mkanganyiko.

Jambo lingine, viongozi wa kisiasa punguzeni kuwapa presha polisi lazima tufahamu kuwa nchi inakuwa na wahalifu wanaongezeka hivyo linavyotokea swala la kupotea kwa mtu msiwe wepesi kunyoosha vidole kwa polisi naona hili linaondoa imani na linaweza kuja kuhatarisha usalama wa nchi

Kuendelea kuwanyooshea polisi mkono kunawezekana kukawapa nguvu wahalifu.

Wananchi tuendele kutambua kuwa
1. Kuna maadui kwenye siasa baina ya mtu na mtu
2. Kuna uadui kwenye mahusiano baina ya mtu na mtu
3. Kuna uadui kwenye biashara baina ya mtu mtu.
4.Kuna uadui wa mtu na utawala. Utawala usiopenda ukweli.
5.kuna uadui wa ndugu kwa ndugu.
6. Kuna uadui wa ndoa baina ya mke na mume.

Hivyo, kuendelea kulinda amani ya taifa ili tulisaidie jeshi la polisi nasi kuwanyooshea vidole zaidi.
 
Tatizo mnachanganya vitu;
1. Madeni ni Bwana harusi, huyu amepatikana Prmba
2. Ulomi ni ishu ya tra, ndiye aliyepata ajali
Naomba ufafanuzi zaidi huyu aliyepatikana Pemba🙏🏿
 
Jeshi la polisi limehusika na mauaji ya watanzania wengi sana na haliwezi kuzikwepa hizi lawama Kwa sababu limehusika Kwa 100%.mfano Sativa alitoa ushuhuda kabisa waliomkamata na sehemu alizokuwa anapelekwa kuwa ni vituo vya polisi (kituo Cha polisi hakifichiki) na baadae kupelekwa pori la katavi na kupigwa risasi Bahati nzuri hiyo risasi haikumuua japo polisi walijua wameua.Tukio lingine ni mzee kibao alikuwa na polisi na matukio mengi tu kama soka,beni saanane,na yule kijana aliyechoma picha ya rais.
 
Bila shaka ni askari wewe...unaezaje kuja kutetea polisi humu?huna macho Wala akili ya kuona uhalisia?
 
Naomba ufafanuzi zaidi huyu aliyepatikana Pemba🙏🏿
Aliyepatikana Pemba kwa mganga kwa ufupi:
1. Ni mkazi wa kigamboni
2. Muuza magari
3. Alifanya harusi akaenda honeymoon, siku ya 4 akamwaga mkewe anaenda kutafuta coaster ya kuwarudisha wakwe Moshi.
4. Hakurejea tena, ikahisiwa ametekwa;

Ukweli;
1. Alikuwa na madeni mengi kiasi akalazimika kuuza gari ya rafiki yake aliloazima kwa ajili ya pilika za harusi.
2. Akakimbilia Pemba kwa mganga, ndiko alipopatikana.
 
Back
Top Bottom