Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto wa Jeshi la Polisi Tanzania, Naibu Kamishna, Mary Nzuki amewataka Askari Polisi wanaofanyakazi Dawati la Usalama Wetu kwanza kuwapa elimu ya afya ya akili na msaada wa kisaikolojia Watoto wahanga wa vitendo vya ukatili.
Akifungua mafunzo ya siku saba ya kuwajengea uwezo wa afya ya akili na msaada wa kisaikolojia jijini Dar es Salaam kwa Askari Polisi wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani alisema elimu na msaada huo unatakiwa kutolewa shuleni na nyumbani kwa kushirikiana na wazazi, walimu na wadau wenye dhamana ya malezi ya watoto.
Alisema mafunzo hayo yatawajengea uwezo wa kiutendaji Askari katika utoaji elimu kwa watoto kwenye shule wanazozifundisha ili wasijiingize kwenye vitendo vya kihalifu pamoja na kutoa msaada wa kisaikolojia kwa watoto wahanga wa vitendo vya ukatili.
Aliwataka washiriki kuwa makini na elimu watakayoipata iwe na ufanisi na kuleta tija kwa Watoto walioko ndani ya jamii.
Alisema Taasisi hizo zimeona ni vyema kushirikiana na Jeshi Polisi kutoa mafunzo hayo kuhakikisha kunakuwa na usalama wa watu kiakili kwani kuna changamoto kuanzia ngazi ya familia, kijamii na kitaifa pia.
Aliongeza kuwa kutokana na changamoto hizo, ujuzi na watakayoipata itamwezesha kila askari kuupelekea kwa Wananchi hususani kuwalinda na kuwapo upendo makundi maalum likiwemo la watoto.
Ufunguzi wa mafunzo hayo, yaliyoandaliwa na Asasi za REPSSI Tanzania kwa kushirikiana SOS Children's Villages na (The Families and Future Coalition of Tanzania (FFCT) ulihudhuriwa pia na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP) Dkt. Lazaro Mambosasa.