Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI
Polisi Dar es Salaam tumejipanga kuimarisha ulinzi na usalama kwa kuweka (deploy) askari wa kutosha katika maeneo yote yanayozunguka uwanja wa Mkapa na barabara zote zinazoingia na kutoka uwanjani hapo.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum linatoa wito kwa wazazi/walezi wanaopenda kwenda na watoto wao uwanjani kuwaangalia kwa ukaribu au kuwaacha kabisa nyumbani ili kuepusha madhara yoyote yanayoweza kujitokeza.
Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wapenzi na mashabiki wa mpira wa miguu kufika uwanjani mapema na kwa wingi, kwani kufika mapema itaepusha msongamano wakati wa kuingia uwanjani milango ya uwanja itafunguliwa mapema na ulinzi utakuwepo wa kutosha na wa uhakika.
Jeshi la Polisi linawataka mashabiki wote kuwa watulivu katika kushangilia mechi hiyo, ikiwa ni pamoja na kuepuka kufanya mambo yafuatayo:-
Pia, Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es Salaam linatarajia kuifunga barabara inayoelekea uwanja wa Mkapa kutokea keko / veta, hivyo mashabiki wanaokwenda uwanjani na magari wanashauriwa kutumia barabara ya Mandela na Chang’ombe.
Aidha, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limeimarisha ulinzi nje na ndani ya viwanja vya Mwalimu Nyerere yanapofanyika maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara, ili kuhakikisha hakuna vitendo vya uhalifu vinavyoweza kujitokeza.
Hivyo basi wananchi wafike kwa wingi kuangalia maonesho hayo, kwani ulinzi ni wa uhakika.
MULIRO J.MULIRO- ACP
KAMANDA WA POLISI,
KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
JESHI LA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM KUIMARISHA ULINZI UWANJA WA BENJAMINI MKAPA KATIKA MCHEZO WA LIGI KUU TANZANIA BARA WA WATANI WA JADI KATI YA SIMBA NA YANGADar es Salaam 01, Julai, 2021
Jeshi la Polisi kanda Maalum Dar es Salaam limejipanga kuimarisha ulinzi na usalama katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya timu ya Simba na Yanga utakaochezwa siku ya Jumamosi ya tarehe 03/07/2021 saa kumi na moja jioni (05:00) katika uwanja wa Benjamini Mkapa.Polisi Dar es Salaam tumejipanga kuimarisha ulinzi na usalama kwa kuweka (deploy) askari wa kutosha katika maeneo yote yanayozunguka uwanja wa Mkapa na barabara zote zinazoingia na kutoka uwanjani hapo.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum linatoa wito kwa wazazi/walezi wanaopenda kwenda na watoto wao uwanjani kuwaangalia kwa ukaribu au kuwaacha kabisa nyumbani ili kuepusha madhara yoyote yanayoweza kujitokeza.
Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wapenzi na mashabiki wa mpira wa miguu kufika uwanjani mapema na kwa wingi, kwani kufika mapema itaepusha msongamano wakati wa kuingia uwanjani milango ya uwanja itafunguliwa mapema na ulinzi utakuwepo wa kutosha na wa uhakika.
Jeshi la Polisi linawataka mashabiki wote kuwa watulivu katika kushangilia mechi hiyo, ikiwa ni pamoja na kuepuka kufanya mambo yafuatayo:-
- kuingia na chupa za aina yoyote uwanjani.
- Kuingia na silaha ya aina yoyote uwanjani.
- Kupaki magari ndani ya uwanja isipokuwa kwa kibali maalum.
- Kukaa sehemu ambazo tiketi zao haziwaruhusu.