Polisi watangaza kufunga barabara ya kuelekea Uwanja wa Mkapa kutokea VETA/Keko

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM KUIMARISHA ULINZI UWANJA WA BENJAMINI MKAPA KATIKA MCHEZO WA LIGI KUU TANZANIA BARA WA WATANI WA JADI KATI YA SIMBA NA YANGA

Dar es Salaam 01, Julai, 2021

Jeshi la Polisi kanda Maalum Dar es Salaam limejipanga kuimarisha ulinzi na usalama katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya timu ya Simba na Yanga utakaochezwa siku ya Jumamosi ya tarehe 03/07/2021 saa kumi na moja jioni (05:00) katika uwanja wa Benjamini Mkapa.

Polisi Dar es Salaam tumejipanga kuimarisha ulinzi na usalama kwa kuweka (deploy) askari wa kutosha katika maeneo yote yanayozunguka uwanja wa Mkapa na barabara zote zinazoingia na kutoka uwanjani hapo.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum linatoa wito kwa wazazi/walezi wanaopenda kwenda na watoto wao uwanjani kuwaangalia kwa ukaribu au kuwaacha kabisa nyumbani ili kuepusha madhara yoyote yanayoweza kujitokeza.

Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wapenzi na mashabiki wa mpira wa miguu kufika uwanjani mapema na kwa wingi, kwani kufika mapema itaepusha msongamano wakati wa kuingia uwanjani milango ya uwanja itafunguliwa mapema na ulinzi utakuwepo wa kutosha na wa uhakika.

Jeshi la Polisi linawataka mashabiki wote kuwa watulivu katika kushangilia mechi hiyo, ikiwa ni pamoja na kuepuka kufanya mambo yafuatayo:-
  • kuingia na chupa za aina yoyote uwanjani.
  • Kuingia na silaha ya aina yoyote uwanjani.
  • Kupaki magari ndani ya uwanja isipokuwa kwa kibali maalum.
  • Kukaa sehemu ambazo tiketi zao haziwaruhusu.

Pia, Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es Salaam linatarajia kuifunga barabara inayoelekea uwanja wa Mkapa kutokea keko / veta, hivyo mashabiki wanaokwenda uwanjani na magari wanashauriwa kutumia barabara ya Mandela na Chang’ombe.

Aidha, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limeimarisha ulinzi nje na ndani ya viwanja vya Mwalimu Nyerere yanapofanyika maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara, ili kuhakikisha hakuna vitendo vya uhalifu vinavyoweza kujitokeza.

Hivyo basi wananchi wafike kwa wingi kuangalia maonesho hayo, kwani ulinzi ni wa uhakika.

MULIRO J.MULIRO- ACP
KAMANDA WA POLISI,
KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM
 
Polisi wahakikishe mageti yanafungwa utopolo watakapoingia uwanjani, wasije kutoroka.
Nadhani hii ndio itakuwa comment ya kijinga zaidi kutumwa JF kwa siku ya leo
Kwa kuongezea nyama kwenye comment ya kijinga dereva wa uto akifika apokonywe funguo na makamanda na arudishiwe mechi ikiisha.
 
Mwalimu wa Wananchi apange kikosi hiki hapa cha ushindi; Mlinda Mlango Farouq Shikalo, no.2 Kibwana Shomari, 3 Adeyun Saleh, 4 Dickson Job, 5 Bakary Mwamnyeto, 6 Mukoko Tonombe, 7 Deus Kaseke, 8 Zawadi Mauya, 9 Yacouba Sogne, 10 Fei Toto,11 Tuisila Kisinda.

Hakika Mikia fc watapoteana.
 
Polisi waandae kikosi maalum cha kuwalinda mashabiki wa Simba kutokana na masumbwi makali yanayorushwaga na mashabiki wa Kidimbwi f.c.
 
Polisi wajinga utafungaje barabara kuanzia Veta, sasa hivi kuna ujenzi unaendelea mbgala foleni ni kubwa halafu wanataka kuongeza foleni
 
Polisi wajinga utafungaje barabara kuanzia Veta, sasa hivi kuna ujenzi unaendelea mbgala foleni ni kubwa halafu wanataka kuongeza foleni
poor reasoning na papara za kupenda kuropoka. sioni mantiki ya kufunga barabara. hii inaoonyesha uwezo mdogo wa kufikiri alionao huyo polisi mkuu wa DSM. Mara nyingi vurugu uwa zinaanzishwa na polisi kwa sababu hizohizo nilizozitaja hapo juu. Polisi waliovaa uniform waende uwanjani kulinda usalama wa raia sio kutazama mpira. Muliro hakikisha polisi wanaoingia uwanjani hakuna anayegeuka kutazama mpira; wote macho yawe kwa watazamaji. Mpira ukiisha imarisha ulinzi barabarani.Kuimarisha ulinzi haina maana kufunga barabara isitumike.
 
Na wale Wezi wa Mandela Road wanao iba Cover za tair mchana kweupe kwenye foleni vipi?mnawashughulikia ?
 
Huku ni kutiana hofu na kuonyesha mabavu yasiyo na maana. Kauli hii ya RPC Murilo itawafanya watu wasiopenda vurugu kutokwenda kabisa uwanjani. Sioni kitu spesheli cha RPC kutoa kauli kama hiyo, huko ni kufanya burdani hiyo kuonekana kuwa ni vita.

Vv
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…