Polisi wateseka na bomu la Arusha bado

Polisi wateseka na bomu la Arusha bado

frema120

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2012
Posts
5,098
Reaction score
1,339
Na Josephat Isango

HARAKATI za Jeshi la Polisi kuishinikiza CHADEMA kuwasilisha ushahidi unaolituhumu jeshi hilo kuhusika na mlipuko wa bomu mkoani Arusha hivi karibuni na kuua watu wanne zimechukua sura mpya.

Jeshi hilo limemuamuru Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kuwasilisha ushahidi unaohusu bomu lililolipuka katika mkutano wa chama hicho uliofanyika viwanja vya Soweto, jijini Arusha Juni 15, mwaka huu.

Ingawa polisi imeendelea na harakati hizo, tayari CHADEMA walishakataa kuutoa ushahidi huo kwa polisi bali wanataka Rais Jakaya Kikwete aunde tume huru ya kijaji itakayosikiliza shauri hilo.
Tanzania Daima Jumapili limefanikiwa kupata nakala yake yenye kumbukumbu ya jalada, AR/IR/6223/2013 ya tarehe 17, Julai 2013.

Barua hiyo inamtaka Mbowe apeleke vielelezo kwa mujibu wa kifungu namba 10 (2) na (2A) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.
Barua hiyo imesainiwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Hussein Laisseri, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai.
"Kutokana na mahojiano uliyofanya na Polisi Mkoa wa Arusha mnamo Juni 20, 2013 kuhusu mauaji yaliyotokana na ulipuaji wa bomu huko Soweto, Arusha ulidai kuwa unao ushihidi unaobainisha wahusika wa tukio hilo.

"Kwa mujibu wa kifungu cha 10 (2) na (2A) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai nchini, sura 20 kama ilivyorekebishwa mwaka 202, unaamriwa kufika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai tarehe 23 Julai, 2013 saa 8 mchana bila kukosa na ulete ushahidi huo, unatahadharishwa kuwa kushindwa au kukataa kufika na kuleta ushahidi huo ni kosa la jinai chini ya sheria iliyotajwa," inaeleza sehemu ya barua hiyo.

Tanzania Daima Jumapili liliwasiliana na baadhi ya wanasheria wa CHADEMA ambao hawakutaka kutajwa majina yao, wamesema kitendo cha polisi kumshinikiza Mbowe kupeleka ushahidi huo ni kuingilia mchakato mwingie wa kisheria.
Walisema kuwa tayari CHADEMA wamepeleka maombi kwa Rais Jakaya Kikwete ili aunde tume huru ya kijaji ambayo mpaka leo hajajibu ombi hilo.
Walibainisha kuwa jeshi hilo wamekosea utaratibu kisheria na kuingilia suala ambalo tayari lipo katika mchakato.

"Haiwezekani kuingilia mchakato mmoja wa kisheria kwa kutumia mchakato mwingine wa kisheria, hii ni sub judice," alisema mmoja wa mawakili.
Wakili huyo alisema hatua ya Jeshi la Polisi nchini kudai ushahidi wa bomu la Arusha kwa nguvu ni ya kushangaza na hawajapata kuitumia kushinikiza masuala mengine.
"Jeshi hilo halijawahi kumlazimisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwataja wauza dawa za kulevya, licha ya kusema majina anayo, hadi sasa hajayaweka hadharani," alisema.

Kauli ya Slaa

Barua hiyo inakuja siku chache baada ya Jeshi la Polisi kumuita na kumhoji kwa maelezo ya onyo kuhusiana na uchochezi Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
Hata hivyo Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alipinga hatua ya polisi kumhoji Mbowe kuhusu ushahidi wa Arusha kwa madai kuwa alichokifanya mwenyekiti wao, huo si msimamo wake bali wa chama.

Dk. Slaa aliweka wazi kuwa kamati kuu ya chama hicho iliamua kuwa ushahidi huo usiwasilishwe polisi kwa sababu ni watuhumiwa katika suala hilo.
"Mbowe hajasema hatatoa ushahidi, atatoa lakini si kwa polisi, tunataka tume huru ya kimahakama ya kijaji, ambayo inapaswa kuundwa na rais, sasa rais hajasema hataunda, Jeshi la Polisi linapoanza kulazimisha ninashindwa kuelewa uwezo wa polisi katika uelewa wa sheria.

"Tumewaeleza polisi kuwa hatutawasilisha ushahidi wetu kwao kwakuwa kwanza sisi tunaamini kuwa wao ni watuhumiwa namba moja," alikaririwa Dk. Slaa.
Dk. Slaa aliongeza kuwa polisi hawakupaswa kumshika Mbowe bali kamati kuu iliyoamua kutoutoa ushahidi huo kwa polisi.

SOURCE: Tanzania Daima
 
Ndio Dr. Kama bwai basi na iwe bwai tu! Kama wao wamechoka na sisi tulishachoka na uharifu wao
 
double standard!! mbona hawakumlazimisha Nchema apeleke mkanda wa ugaidi wa CDM, mpaka pale Ludo, akishirikiana na Majid na Michuzi waalipouweka mtandaoni kupitia ID ya "BUKOBA BOY"
 
kwa mambo kama haya ya kipuuzi yanayoendelea, eti tuweke utaifa mbele kupambana na Kagame,kisa kamtukana JK "idiot"
 
hii ndo double standard, Polisi lazima wajue kuwa wao ndo watuhumiwa, na mtuhumiwa hapaswi kupewa ushahidi unaomhusu, na Rais wa CCM kama yeye na chama chake hawausiki kwa nini asiunde Tume huru ya kimahakama? shame on you dhaifu kiongozi
 
Hapa ndiyo huwa nawakubali CHADEMA,wanajua kabisa kwa hilo Serikali haitafurukuta maana haitatokea Rais kuunda Tume huru,narudia tena haitatokea.
 
Hapa ndiyo huwa nawakubali CHADEMA,wanajua kabisa kwa hilo Serikali haitafurukuta maana haitatokea Rais kuunda Tume huru,narudia tena haitatokea.
[MENTION][JFMP3][/JFMP3][/MENTION]

Mbona kuna tume nyingi zimeundwa pamoja nakwamba matokeo yake bado nikitendawili, inakuaje hii wanapata kigugumizi kuiunda?
 
Naona Police wanasogelea shimo kimgongomgongo na wakiishaingia hawatatoka na kama watatoka basi watatoka wachafu
 
Hapa ndiyo huwa nawakubali CHADEMA,wanajua kabisa kwa hilo Serikali haitafurukuta maana haitatokea Rais kuunda Tume huru,narudia tena haitatokea.
Kuna mambo mawili hapa:
Kwanza JK anajiona kwa Superiority na power aliyo nayo hawezi kuelekezwa, kupangiwa au hata kushauriwa jambo na wapinzani wake, na kisha akatekeleza. Anahisi atapunguza heshima anayohisi kuwa nayo.

Pili ni kwamba anajua kuwa kuna ukweli katika madai ya Cdm, hivyo kuunda tume hiyo ni kama kujikaanga kwa mafuta yake mwenyewe!
The Arusha scam is his own baby, of whom he cant jeorpadize!
 
tanzania rais hatuna rais gan asiyekua na maamnzi kwa vitu vya msingi lakini.kwa nn hataki kujibu hiyo barua kwa nin? anakwepa kwa maana hiyo yeye kama mkubwa wa kazi imemshinda TZ dhaifu kwa viongozi dhaifu hatuta endelea.
 
Polisi wa Tanzania wamekubuhu kwa uhalifu
 
[TD="bgcolor: #FFFFFF"] HARAKATI za Jeshi la Polisi kuishinikiza CHADEMA kuwasilisha ushahidi unaolituhumu jeshi hilo kuhusika na mlipuko wa bomu mkoani Arusha hivi karibuni na kuua watu wanne zimechukua sura mpya.

Jeshi hilo limemuamuru Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kuwasilisha ushahidi unaohusu bomu lililolipuka katika mkutano wa chama hicho uliofanyika viwanja vya Soweto, jijini Arusha Juni 15, mwaka huu.

Ingawa polisi imeendelea na harakati hizo, tayari CHADEMA walishakataa kuutoa ushahidi huo kwa polisi bali wanataka Rais Jakaya Kikwete aunde tume huru ya kijaji itakayosikiliza shauri hilo.
Tanzania Daima Jumapili limefanikiwa kupata nakala yake yenye kumbukumbu ya jalada, AR/IR/6223/2013 ya tarehe 17, Julai 2013.

Barua hiyo inamtaka Mbowe apeleke vielelezo kwa mujibu wa kifungu namba 10 (2) na (2A) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.
Barua hiyo imesainiwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Hussein Laisseri, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai.
“Kutokana na mahojiano uliyofanya na Polisi Mkoa wa Arusha mnamo Juni 20, 2013 kuhusu mauaji yaliyotokana na ulipuaji wa bomu huko Soweto, Arusha ulidai kuwa unao ushihidi unaobainisha wahusika wa tukio hilo.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 10 (2) na (2A) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai nchini, sura 20 kama ilivyorekebishwa mwaka 202, unaamriwa kufika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai tarehe 23 Julai, 2013 saa 8 mchana bila kukosa na ulete ushahidi huo, unatahadharishwa kuwa kushindwa au kukataa kufika na kuleta ushahidi huo ni kosa la jinai chini ya sheria iliyotajwa,” inaeleza sehemu ya barua hiyo.

Tanzania Daima Jumapili liliwasiliana na baadhi ya wanasheria wa CHADEMA ambao hawakutaka kutajwa majina yao, wamesema kitendo cha polisi kumshinikiza Mbowe kupeleka ushahidi huo ni kuingilia mchakato mwingie wa kisheria.
Walisema kuwa tayari CHADEMA wamepeleka maombi kwa Rais Jakaya Kikwete ili aunde tume huru ya kijaji ambayo mpaka leo hajajibu ombi hilo.
Walibainisha kuwa jeshi hilo wamekosea utaratibu kisheria na kuingilia suala ambalo tayari lipo katika mchakato.

“Haiwezekani kuingilia mchakato mmoja wa kisheria kwa kutumia mchakato mwingine wa kisheria, hii ni sub judice,” alisema mmoja wa mawakili.
Wakili huyo alisema hatua ya Jeshi la Polisi nchini kudai ushahidi wa bomu la Arusha kwa nguvu ni ya kushangaza na hawajapata kuitumia kushinikiza masuala mengine.
“Jeshi hilo halijawahi kumlazimisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwataja wauza dawa za kulevya, licha ya kusema majina anayo, hadi sasa hajayaweka hadharani,” alisema.

Kauli ya Slaa

Barua hiyo inakuja siku chache baada ya Jeshi la Polisi kumuita na kumhoji kwa maelezo ya onyo kuhusiana na uchochezi Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
Hata hivyo Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alipinga hatua ya polisi kumhoji Mbowe kuhusu ushahidi wa Arusha kwa madai kuwa alichokifanya mwenyekiti wao, huo si msimamo wake bali wa chama.

Dk. Slaa aliweka wazi kuwa kamati kuu ya chama hicho iliamua kuwa ushahidi huo usiwasilishwe polisi kwa sababu ni watuhumiwa katika suala hilo.
“Mbowe hajasema hatatoa ushahidi, atatoa lakini si kwa polisi, tunataka tume huru ya kimahakama ya kijaji, ambayo inapaswa kuundwa na rais, sasa rais hajasema hataunda, Jeshi la Polisi linapoanza kulazimisha ninashindwa kuelewa uwezo wa polisi katika uelewa wa sheria.

“Tumewaeleza polisi kuwa hatutawasilisha ushahidi wetu kwao kwakuwa kwanza sisi tunaamini kuwa wao ni watuhumiwa namba moja,” alikaririwa Dk. Slaa.
Dk. Slaa aliongeza kuwa polisi hawakupaswa kumshika Mbowe bali kamati kuu iliyoamua kutoutoa ushahidi huo kwa polisi.

[TD="bgcolor: #FFFFFF"]
Polisi wateseka na bomu la Arusha

na Josephat Isango
Tanzania Daima

[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #FFFFFF, align: center"][/TD]
[/TD]
 
Tunakoelekea siko police wamechoshwa na utawala uliopo wanaona ni heri wachochee vurugu
 
Kuna mambo mawili hapa:
Kwanza JK anajiona kwa Superiority na power aliyo nayo hawezi kuelekezwa, kupangiwa au hata kushauriwa jambo na wapinzani wake, na kisha akatekeleza. Anahisi atapunguza heshima anayohisi kuwa nayo.

Pili ni kwamba anajua kuwa kuna ukweli katika madai ya Cdm, hivyo kuunda tume hiyo ni kama kujikaanga kwa mafuta yake mwenyewe!
The Arusha scam is his own baby, of whom he cant jeorpadize!
kuhusu kushauriwa nakataa, kwani amesha kubali lakatiba mpya ambayo ilikuwa hoja ya wapinzani, hilo la pili kwa asilimia kubwa laweza kuwa sahihi anaogopa kujishika utumbo kwani mwigulu ana back up za ikulu
 
Mwuaji anapokulazimisha ushahidi wa uuaji wake kwa kusudi la kuuchunguza na kuupeleka mahakamani ili ashitakiwe kwa uuaji pale mwuaji mwenyewe akiona kuwa ule ushahidi unatosha kumtia hatiani.Hivi jambo hili linawezekana kutendwa na yeyote kweli hata kwa kuota tu? Nadhani mmbwa wetu siku hizi wana mtindio wa akili na ndio sababu wanabweka hata wakiona kivuli tu. Bahati mbaya kwao ugonjwa huu una kinga tu. Mbaya zaidi bwana zao wamelewa chakari kilevi kibaya cha madaraka kiasi kwamba sasa wamechoka hivi kwamba hawajimudu kwa hoja zaidi ya kuachia kamba za mmbwa na kuwaamuru wabweke na kung'ata watu hovyo. Jihadhalini na mmbwa, jilindeni na mbweha. Asalaam aleykum.
 
Back
Top Bottom