Polisi wathibitisha Katibu wa Masanja kajinyonga. Mke wa Masanja alienda kwake kumuonya asiwe anamtumia meseji za mapenzi

Polisi wathibitisha Katibu wa Masanja kajinyonga. Mke wa Masanja alienda kwake kumuonya asiwe anamtumia meseji za mapenzi

'hataki uhusiano naye na asimtumie sms za mapenzi','marehemu alikuwa akiomba mahusiano ya kimapenzi','walienda nyumbani kwa marehemu kumueleza kuwa hataki meseji za aina hiyo na hataki uhusiano'.Kwa maelezo haya inaonyesha jamaa alikuwa anataka uhusiano wa kimapenzi na mke wa Masanja,sasa kwa mtiririko huu inaoyesha hawakuwa wapenzi,na huyu jamaa baada ya kuona amekataliwa akajua habari itamfikia mwenye mali hivyo akaamua kujinyonga,CASE CLOSED...
Wakulungwa hawataki hii ripoti
 
Achaneni na wake wa watu wenye pesa, la sivyo vifo vyenu vitasemekana

Alijinyonga
Aligongwa na Gari
Alidondoka Ghafla
Alidondokewa na Kitu,nk

Mtaondoka bila kujua mliondokaje,Pesa itabaki kuitwa Pesa

Ukiona unanyege pambana na wake za maskini achaneni kbs

na wake za watu wanaojiweza,shauri lenu,Mwenzenu ndio huyo "kashajinyonga"
 
Kupitia Clouds FM Polisi jijini DSM wamethibitisha kuwa katibu wa kanisa la Masanja amefariki kwa kujinyonga kwa uchunguzi wa awali.

Kamanda anasema ni kweli siku moja kabla ya kifo cha Katibu, mke wa Masanja alienda nyumbani kwa Katibu akiwa na mama mtu mzima kumwambia hataki uhusiano naye na asimtumie sms za mapenzi. Kamanda akaendelea kusema ni kweli kulikuwa na mawasiliano kati ya marehemu Katibu na mke wa Masanja.

Polisi wanasema kwa uchunguzi wa awali unaonyesha Katibu alijinyonga kwa sababu ya mapenzi lakini bado wanaendelea na uchunguzi.

========================

Polisi wamesema uchunguzi wa awali yanaonesha Joas Steven alipata mfadhiko na kujiua kwa kujinyonga.

Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Maalum Dar es Salaam, Muliro Jumanne amesema pia mawasiliano kati ya marehemu na anayedaiwa kuwa ni mke wa Masanja (Emmanuel Mgaya) yalifanyika kwa simu.

Amesema “Mawasiliano yanaonesha marehemu alikuwa akiomba mahusiano ya kimapenzi, pia siku moja kabla ya tukio mke wa Masanja akiwa na mwanamke mwingine walienda nyumbani kwa marehemu kumueleza kuwa hataki meseji za aina hiyo na hataki uhusiano.”

Kamanda Muliro ameongeza, “Mtiririko wa visa hivyo unatoa nafasi kuwa alipata mfadhaiko akajinyonga, lakini hata hivyo bado uchunguzi unaendelea kwa kuwa huo ni ushahidi wa awali.”


View attachment 2376847
Mchungaji Masanja Kulia akiwa na Marehemu.

View attachment 2376956
Sauti ya Kamishna wa Polisi (ACP) Muliro Jumanne

Kama Mke wa Masanja ni Msukuma basi huyo ni mke wa wengi.​

 
Mwanamke/mke ukimsumbua sana kumtongoza na kama Ana mme!
Huwa anakutengenezea mtego akishirikiana na mme wake+wazee
Sasa kwanini mke wa mchungaji asingechukua hatua hiyo
Ni kama alikuwa anapenda

Ova
Kila mtu ana namna yake ya kutatua changamoto. Sasa mama mtumishi yeye kaona hiyo ya kutafuta mama anayeheshimika hapo kanisani amsaidie kufikisha ujumbe inafaa. hatuwezi kumlaumu mama mtumishi kwa hilo.
Inaelekea dogo hakuwa mzima kisaikologia na afya ya akili. Hata kama alikuwa mpenzi wake wa siku nyingi na bado alikuwa anaendelea kuibia ibia, alipaswa kujua kuwa sasa kaolewa tena na mkuu wake wa kiroho na akubali yaishe. Bila shaka watu kama hawa, ndio angepata mwanya angeweza hata kumuua huyu mama ili wakose wote.
 
Nitakuwa wa Mwisho kuamini kuwa Mtu anaweza kujinyonga kwa ajili ya Mke wa Mtu. Aiseee hapana, hiyo haiwezekani.

Kujinyonga kwa Mke wako naweza nikakubali, ila kwa mke wa mtu. Hiyo kwangu ni Big no
Nakazia hapa
 
Masanja ushamba ulizidi, watu tuna mademu wakali tumetulia tu, nani anamjua mke wa Mpoki au Jotti, watoto wa mjini marufuku kupost wake zao mitandaoni.
Uposti usi posti anaweza ibiwa vile vile sasa huyo katibu si kila siku alikua anamuona
 
Hapana, inamlinda mchungaji na mkewe, maana polisi wanasema mama mchungaji akisindikizwa na mtu mwingine walienda kwa marehemu kumwambia aache kumtumia sms za mapenzi kwa yeye(mama mchungaji) ni mke wa mtu tayari. So inaonekana jamaa ndio kwanza alikuwa anatongoza hajala tunda
Hujauelewa mchezo nadhani
 
Kuna taarifa zinasambaa kwamba Masanja na mkewe watakamatw kwa ajili ya uchunguzi zaidi kuhusiana na kifo cha katibu wake wa kanisa

Inasemakana kwamba katibu uyo a kanisa la masanja wala hakujinyonga bali alinyongwa na kisha kuzusha kwamba amejinyonga

Nb tayari mwili wa Marehemu umeishazikwa, mwili huo umezikwa jana
Mbona mapema sana
 
Polisi wanasema marehem ndio alikua anaomba mahusiano ya kimapenzi (anamtongoza) lakin walimwengu wame conclude walikua wapenzi duh hatar kwa kujiongeza
Polisi na walimwengu wanaongea lugha moja, hujaielewa tu ile ya polisi
 
'hataki uhusiano naye na asimtumie sms za mapenzi','marehemu alikuwa akiomba mahusiano ya kimapenzi','walienda nyumbani kwa marehemu kumueleza kuwa hataki meseji za aina hiyo na hataki uhusiano'.Kwa maelezo haya inaonyesha jamaa alikuwa anataka uhusiano wa kimapenzi na mke wa Masanja,sasa kwa mtiririko huu inaoyesha hawakuwa wapenzi,na huyu jamaa baada ya kuona amekataliwa akajua habari itamfikia mwenye mali hivyo akaamua kujinyonga,CASE CLOSED...
Mmetumwa ku-clear the air

Hawa walikuwa wapenzi
 
Back
Top Bottom