Polisi wathibitisha Katibu wa Masanja kajinyonga. Mke wa Masanja alienda kwake kumuonya asiwe anamtumia meseji za mapenzi

Polisi wathibitisha Katibu wa Masanja kajinyonga. Mke wa Masanja alienda kwake kumuonya asiwe anamtumia meseji za mapenzi

Kupitia Clouds FM Polisi jijini DSM wamethibitisha kuwa katibu wa kanisa la Masanja amefariki kwa kujinyonga kwa uchunguzi wa awali.

Kamanda anasema ni kweli siku moja kabla ya kifo cha Katibu, mke wa Masanja alienda nyumbani kwa Katibu akiwa na mama mtu mzima kumwambia hataki uhusiano naye na asimtumie sms za mapenzi. Kamanda akaendelea kusema ni kweli kulikuwa na mawasiliano kati ya marehemu Katibu na mke wa Masanja.

Polisi wanasema kwa uchunguzi wa awali unaonyesha Katibu alijinyonga kwa sababu ya mapenzi lakini bado wanaendelea na uchunguzi.

========================

Polisi wamesema uchunguzi wa awali yanaonesha Joas Steven alipata mfadhiko na kujiua kwa kujinyonga.

Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Maalum Dar es Salaam, Muliro Jumanne amesema pia mawasiliano kati ya marehemu na anayedaiwa kuwa ni mke wa Masanja (Emmanuel Mgaya) yalifanyika kwa simu.

Amesema “Mawasiliano yanaonesha marehemu alikuwa akiomba mahusiano ya kimapenzi, pia siku moja kabla ya tukio mke wa Masanja akiwa na mwanamke mwingine walienda nyumbani kwa marehemu kumueleza kuwa hataki meseji za aina hiyo na hataki uhusiano.”

Kamanda Muliro ameongeza, “Mtiririko wa visa hivyo unatoa nafasi kuwa alipata mfadhaiko akajinyonga, lakini hata hivyo bado uchunguzi unaendelea kwa kuwa huo ni ushahidi wa awali.”


View attachment 2376847
Mchungaji Masanja Kulia akiwa na Marehemu.

View attachment 2376956
Sauti ya Kamishna wa Polisi (ACP) Muliro Jumanne​
Dunia ndivyo ilivyo
 
Watu waelewe hakuna mtu asiyezingua. Watu tuko na madhambi kibao.

Angefukuzwa kanisa au kutengwa na waumini wenzake na kanisa pia ila maisha yangesonga tu.

Hamnaga sababu ya kujiua
 
Back
Top Bottom