Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limeona taarifa inayo sambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kukamatwa kwa Lucy Shayo.
Tunasititiza kuwa ni kweli Lucy Simon Shayo (32), mkulima na mkazi wa Ruaha Mbuyuni Mkoa wa Iringa, pamoja na Stephan Godwel Simchimba (41), mkazi wa Tanga, wamekamatwa na Jeshi la Polisi katika majukumu yake ya kawaida ya kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu.
Uchunguzi wa kina unaendelea, na taarifa rasmi kamili itatolewa kwa umma mara baada ya taratibu za awali kukamilika.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu na kutokuwa na wasiwasi, kwani Jeshi la Polisi linafanya kazi zake kwa kuzingatia weledi, haki, nidhamu na uadilifu kwa mujibu wa sheria za nchi.
Imetolewa na;
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Morogoro.