Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mwenyekiti wa Taasisi ya Taifa ya Madereva Tanzania (TATAMATA), Yohana Mwanyaga, amesema Jeshi la Polisi limethibitisha kuwa Rodgers Kateba, ambaye awali aliripotiwa kupotea, yuko hai na anashikiliwa na jeshi hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari , Novemba 1, 2026, Mwanyaga amesema baada ya taasisi hiyo kuzungumza na vyombo vya habari Oktoba 29, 2026, kuhusu kutafuta Kateba, Oktoba 31,2026 walipokea simu kutoka Jeshi la Polisi na kufika Kituo Kikuu cha Polisi (Central), ambako walikutana na kamanda wa polisi.
Kwa mujibu wa Mwanyaga, walielezwa kuwa Kateba yuko salama na hajapigwa, huku polisi wakisema wanatarajia kumfikisha mahakamani ndani ya siku mbili zijazo kutokana na tuhuma zinazomkabili. Hata hivyo, Mwanyaga hakufafanua tuhuma hizo, akisema hawezi kuzitaja kwa wakati huo.
Pia soma: Dereva Kateba atekwa na watu wasiojulikana, Madereva wataka apatikane akiwa hai
Amesema taarifa hiyo imepunguza hofu iliyokuwepo miongoni mwa madereva kuhusu usalama wa Kateba, huku akieleza kuwa taarifa zaidi kuhusu hatua zinazofuata zitapa