Polisi watoa taarifa kifo cha Ulomi wasema alifariki kwa ajali ya pikipiki

Alifariki kwa pikipiki Toka 11/12/2024 hajulikani alipo je hiyo ajali ilitokea maporini ambapo mwili haukuonekana mpaka leo?
Maswali ni mengi sana, kwa ulimwengu huu wa mitandao, mtu anatafutwa tangu tarehe 11, hao wasamaria wema inamaana hawakutambua hiyo picha wakatoa taarifa mapema kwamba alipata ajali mbaya?

Labda tuendelee kusubiri uchunguzi wa kina kama taarifa inavyodai.
 
Labda wasamaria wema, zahanati na hospital wote hawakupata taarifa ya kupotea kwake au hawakumtambua!
Kama ni hivyo basi inazidi kutia wasiwasi. Alipokelewa hapo dispensary akupelekwa Mwananyamala bila polisi kutaarifiwa? Ajali haikuripotiwa polisi? Mtu akipotea tena akiwa na pikipiki, sehemu za kwanza kutafuta ni hospital na vyumba vya maiti. Ndugu zake na polisi muda wote huu hawakuwa wameulizia? Je, hospital zinapopokea mtu ambaye hajitambui na akafariki, hawatoi taarifa hospital?
 
Sasa we unataka wafanyaje kama mtu ameshakufa
 
Utata mtupu.
 
Je hakuwa na vitambulisho?
Je hakuwa na simu mfukoni? Namba ya simu iliyo mfukoni ilikuwa na line iliyosajiliwa kwa jina lipi?
Je namba ya pikipiki aliyokuwa anaiendesha ilikuwa imesajiliwa kwa jina lipi?
 
Hospital wakipokea mtu wa ajali ambaye hajitambui na akafariki huwa hawatoi taarifa polisi? Huyu kapotea tangu tarehe 11.
 
#HABARI Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema kuwa Daisle Simion Ulomi, aliyekuwa ameripotiwa kwamba amepotea, alifariki dunia baada ya kupata ajali mbaya na pikipiki aliyokuwa akiitumia siku ya Desemba 11, 2024.

Taarifa hiyo imetolewa leo Desemba 16, 2024 na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo SACP Jumanne Muliro ambapo ameeleza kuwa tarehe 11 Desemba, 2024 Jeshi hilo lilipata taarifa ya kupotea kwake na ndugu hawakuwa wanampata kwenye mawasiliano ya simu, baada ya yeye kuondoka ofisini kwake Sinza na kudai anaelekea Temeke kufuatilia makontena yake ya biashara.

"Ulomi aliondoka eneo lake huku akitumia pikipiki namba MC 415 DQC aliyokuwa akiendesha mwenyewe, ufuatiliaji umefanyika kwa kushirikiana na ndugu na kubainika kuwa Ulomi alipelekwa kituo cha afya cha Makuburi Ubungo External mchana wa tarehe 11 Desemba, 2024 baada ya kupata ajali mbaya na pikipiki aliyokuwa akiitumia, wasamaria wema walimsadia kumpeleka kwenye kituo hicho akiwa hajitambui na hakuwa na kitambulisho chochote," imeeleza taarifa ya Kamanda Muliro.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa, " Baadae alipelekwa Mwananyamala hospitali na ikabainika tayari alikuwa amefariki na maiti yake kuhifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo kama mtu asiyefahamika akisubiri kutambuliwa na ndugu, ndugu tayari wameutambua mwili huo ukiwa na majeraha maeneo mbalimbali ya mwili. Aidha, Pikipiki aliyopata nayo ajali pia imepatikana ikiwa imeharibika. uchunguzi zaidi wa ajali hiyo unaendelea na taarifa zaidi itatolewa,".

#EastAfricaRadio
 
Ja hakuwa na vitambulisho? Je namba ya pikipiki aliyokuwa anaiendesha ilikuwa imesajiliwa kwa jina lipi?
Wanadai hakuwa na kitambulisho. Ila bado kuna utata mwingi. Mimi nilidhani mtu mwenye pikipiki asiporudi nyumbani tena jiji kama Dar, jambo la kwanza kuja kichwani ni ''ajali'' na kujaribu kutafuta hospital zote!
 
Wanadai hakuwa na kitambulisho. Ila bado kuna utata mwingi. Mimi nilidhani mtu mwenye pikipiki asiporudi nyumbani tena jiji kama Dar, jambo la kwanza kuja kichwani ni ''ajali'' na kujaribu kutafuta hospital zote!
Hatari sana.
 

Wamerusha taarifa ya polisi ya Temeke.
Sasa swali ni je ajali iwapo alipata Temeke ndipo wakaamua apelekwe hospital ya makuburi ma bibi badala ya Temeke hospital ambayo ilikuwa karibu zaidi ??
 
Tajiri mkubwa kama Ulomi anapanda pikipiki?! Wewe ukiambiwa Dewji amepata ajali ya pkpk utaamini. Polisi acheni kuwaona watu wote ni wajinga.
 
Hospital wakipokea mtu wa ajali ambaye hajitambui na akafariki huwa hawatoi taarifa polisi? Huyu kapotea tangu tarehe 11.
Polisi na Hospitali wanafanya kazi kwa ushirikiano tena wa karibu pale inapohitajika.
Tatizo ni kwamba mifumo yote ipo corrupt kwa maslahi ya wazito kadhaa kwahy hakuna uwazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…