Pre GE2025 Polisi wilaya ya Arusha, waaswa kujipanga kusimamia uchaguzi mkuu

Pre GE2025 Polisi wilaya ya Arusha, waaswa kujipanga kusimamia uchaguzi mkuu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Jeshi la Polisi Wilaya ya Arusha limehimizwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi na kulinda raia na mali zao huku likikumbishwa kutambua kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi ambapo Jeshi hilo ndilo lenye dhamana ya kuhakikisha ulinzi na usalama wakati wote wa uchaguzi na baada ya uchaguzi kukamilika.

Hayo yamebainishwa leo Februari 28, 2025 na Mwenyekiti wa kamati ya Usalama Wilaya ya Arusha ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Joseph Mkude ambapo amesema Jeshi la Polisi Wilayani humo linayo dhamana ya kuhakikisha ulinzi na usalama unaendelea kuwepo muda wote kutokana na asili ya Wilaya hiyo ambayo inatembelewa na wageni wengi wa ndani na nje ya nchi.

Pia soma: LGE2024 - Special Thread: Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Ameongeza kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi ambapo amebainisha kuwa katika kipindi hicho mambo mengi huibuka huku akilitaka Jeshi la Polisi wilayani humo kuhakikisha linadhibiti vitendo vyote vya uvunjifu wa amani kwa kipindi chote.

 
Back
Top Bottom