Jeshi la Polisi Wilaya ya Arusha limehimizwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi na kulinda raia na mali zao huku likikumbishwa kutambua kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi ambapo Jeshi hilo ndilo lenye dhamana ya kuhakikisha ulinzi na usalama wakati wote wa uchaguzi na baada ya uchaguzi kukamilika.
Hayo yamebainishwa leo Februari 28, 2025 na Mwenyekiti wa kamati ya Usalama Wilaya ya Arusha ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Joseph Mkude ambapo amesema Jeshi la Polisi Wilayani humo linayo dhamana ya kuhakikisha ulinzi na usalama unaendelea kuwepo muda wote kutokana na asili ya Wilaya hiyo ambayo inatembelewa na wageni wengi wa ndani na nje ya nchi.
Ameongeza kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi ambapo amebainisha kuwa katika kipindi hicho mambo mengi huibuka huku akilitaka Jeshi la Polisi wilayani humo kuhakikisha linadhibiti vitendo vyote vya uvunjifu wa amani kwa kipindi chote.