JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Jeshi la Polisi nchini limezuia mikutano ya hadhara ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyopangwa kufanyika wilaya ya Ngorongoro, mkoani Arusha kuanzia Agosti 29.2024 hadi Septemba 15.2024, mikutano iliyotarajiwa kuongozwa na Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa CPA Amos Gabriel Makala
Taarifa ya Jeshi hilo iliyotumwa kutoka ofisi ya Mkuu wa Polisi (OCD) wilaya ya Ngorongoro kwenda ofisi kuu ya CCM wilaya ya Ngorongoro ikijibu barua ya CCM yenye kumbukumbu namba CCM/NGN/OFU/10/311/VOL. 111/37 ya Agosti 23.2024 imeeleza kuwa mikutano hiyo haijaruhusiwa.
Pia soma: Polisi yazuia Mkutano wa ACT Wazalendo, yasema mikutano ya hadhara na ndani imezuiliwa
Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa kutokana na shughuli za kuimarisha usalama zinazoendelea katika maeneo hayo (Ngorongoro) Jeshi la Polisi limesitisha mikutano, mikusanyiko ya watu katika maeneo hayo nk, hadi hapo itakavyoelekezwa vinginevyo siku za usoni
Taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi iliyotolewa Agosti 27.2024 imesainiwa na SSP L.N.Ncheyeki ambaye ni Mkuu wa Polisi wilaya ya Ngorongoro