Pre GE2025 Polisi yaizuia Mkutano wa CCM kufanyika Ngorongoro

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607


Jeshi la Polisi nchini limezuia mikutano ya hadhara ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyopangwa kufanyika wilaya ya Ngorongoro, mkoani Arusha kuanzia Agosti 29.2024 hadi Septemba 15.2024, mikutano iliyotarajiwa kuongozwa na Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa CPA Amos Gabriel Makala

Taarifa ya Jeshi hilo iliyotumwa kutoka ofisi ya Mkuu wa Polisi (OCD) wilaya ya Ngorongoro kwenda ofisi kuu ya CCM wilaya ya Ngorongoro ikijibu barua ya CCM yenye kumbukumbu namba CCM/NGN/OFU/10/311/VOL. 111/37 ya Agosti 23.2024 imeeleza kuwa mikutano hiyo haijaruhusiwa.

Pia soma: Polisi yazuia Mkutano wa ACT Wazalendo, yasema mikutano ya hadhara na ndani imezuiliwa

Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa kutokana na shughuli za kuimarisha usalama zinazoendelea katika maeneo hayo (Ngorongoro) Jeshi la Polisi limesitisha mikutano, mikusanyiko ya watu katika maeneo hayo nk, hadi hapo itakavyoelekezwa vinginevyo siku za usoni

Taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi iliyotolewa Agosti 27.2024 imesainiwa na SSP L.N.Ncheyeki ambaye ni Mkuu wa Polisi wilaya ya Ngorongoro
 

Attachments

  • GWDGAQZWQAEqdci.jpg
    324.9 KB · Views: 7
Katibu wa NEC, itikadi na uenezi CCM ndugu Amos Makalla amethibitisha kupokea barua kutoka jeshi la polisi Ngorongoro ya kukataa maombi ya kufanya mikutano ya hadhara wilayano humo na kubainisha kua chama hicho kipokea na kuheshimu barua hiyo na sababu za kukataliwa kufanya mkutano. Hata hiyo Makalla amesema kuwa atafanya ziara zake Longido Monduli na Karatu.
 
CCM wana akili fupi sana kama kima!!
 
Tunaijua hii
 

Kwamba ni Lucas Mwashambwa, Tlaatlaah au johnthebaptist ndiyo waliopiga marufuku?

Tufanye tumekubali.

Hongereni!
 
Hii ni janja ya ccm. Yote ni kuweka mazingira ya kuwazuia vyama vya upinzani visifike huko. Inatengeneza mazingira ya kuwaaminisha watu kuwa hata wao CCM walizuiliwa huko kwa sababu za usalama.
 
Naipongeza sana CCM kwa kutii , kuheshimu na kufuata maelekezo ya jeshi la polisi. Wangekuwa ni Ma CHADEMA ungeona wanaanza kuropoka ropoka na kutoa matamko ya uchochezi na mavurugu tu.
 
Naipongeza sana CCM kwa kutii , kuheshimu na kufuata maelekezo ya jeshi la polisi. Wangekuwa ni Ma CHADEMA ungeona wanaanza kuropoka ropoka na kutoa matamko ya uchochezi na mavurugu tu.

Kwamba ujipige marufuku, kisha utii, halafu ujipongeze?

Kumbe offside ni kwenye kabumbu tu?

Kwa kumuonaje, nani vile ... ?
 
Itakuwa walikubaliana waombe kibali kisha wawakatalie ili ionekane haki inatendeka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…