Polisi yamshikilia Mchungaji EAGT tuhuma za kubaka, kumpa mimba Mwanafunzi

Polisi yamshikilia Mchungaji EAGT tuhuma za kubaka, kumpa mimba Mwanafunzi

Tuhuma kwa viongozi wa kidini ni vyema zikachukuliwa kwa tahadhari ya hali ya juu.
Wakati mwingine ni chuki za kuwaharibia tu.
Hii nimeshuhudia mara kadhaa na wapanga njema meisho huishia kuaibika.
Japo wapo wengi ssna wenye tabia hizi pia

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli lakini awa viongozi wa dini wanapotoa huduma iwe kwa makundi sio kwa mtu mmojammoja.
 
Tuhuma kwa viongozi wa kidini ni vyema zikachukuliwa kwa tahadhari ya hali ya juu.
Wakati mwingine ni chuki za kuwaharibia tu.
Hii nimeshuhudia mara kadhaa na wapanga njema meisho huishia kuaibika.
Japo wapo wengi ssna wenye tabia hizi pia

Sent using Jamii Forums mobile app
USPOTEZEE WEWEE. ALAAA?!!
 
Polisi wilayani Kisarawe mkoani Pwani, inamshikilia Mchungaji wa kanisa la EAGT la Mtamba, Shauri Steven kwa tuhuma za kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi akimlaghai kupitia huduma ya maombi

Dar es Salaam. Mchungaji wa Kanisa la EAGT la Mtamba wilayani Kisarawe mkoani Pwani, Shauri Steven anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi wa darasa la tano.

Mwanafunzi huyo amebakwa na kupewa mimba wakati takwimu zikionyesha mwanafunzi mmoja kati ya watatu amekatisha masomo kwa mimba au ndoa za utotoni.

Akizungumza na Mwananchi jana Jumanne Desemba 17, 2019 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amesema sababu za mchungaji huyo kubaka na kumpa mwanafunzi mimba ni tamaa za mwili.

Alisema mchungaji huyo alifanikiwa kumlaghai mwanafunzi kwa madai ya kumfanyia huduma ya maombi.

Jokate ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya Kisarawe alisema Desemba 12, 2019 mwalimu wa shule ya msingi Mtamba, Justine Mrutu aligundua mwanafunzi huyo mjamzito.

"Alimlaghai kupitia mbinu ya maombi, mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani," alisema Jokate.

Chanzo: Mwananchi
Ikibainika kweli wampige nyundo 30 zinamtosha akitoka kachakaa
 
Back
Top Bottom