Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Limesema hivyo kutokana na taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Zitto kuwa anazo taarifa muhimu zinazoweza kusaidia kukamatwa kwa mtu huyo anayejiita Kigogo.
Kwa muda mrefu kumekuwa na akaunti ya mtandao wa kijamii wa Twitter, inayotumia jina la Kigogo na sura ya mwanamuziki wa Hip Hop kutoka Marekani, Jay Z.
Akaunti hiyo hutoa tuhuma mbalimbali kwa serikali na kukosoa mara kwa mara mambo yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Hatua hiyo imekuwa ikichukuliwa ni uhalifu, hasa kutokana na shutuma nzito anazozitoa ‘Kigogo’ huyo kwa Serikali ya Rais John Magufuli.
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola aliwahi kutoa tamko kupitia vyombo vya habari kuwa Kigogo huyo anakaribia kukamatwa.
Wiki iliyopita, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini katika akaunti yake ya Twitter, aliweka sura ya mtu aliyemtambulisha kwa jina la Didier Abdallah Mlawa anayeishi Uingereza, huku akisisitiza kuwa mtu huyo ndiye anamiliki akaunti hiyo ya Kigogo, inayoichafua serikali.
Hatua ya Zitto kufikia uamuzi huo, imetokana na wawili hao kutofautiana, ambapo katika majibizano yao, Zitto alibainisha kuwa Kigogo kwa sasa amekuwa akitaka kukabiliana na yeye, kwa kuwa ni pingamizi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku Zitto akijinadi kuwa hawezi kulaza damu katika kukabiliana na mtu kama Kigogo.
Zitto alifikia hatua ya kumtaka Kigogo, arejee nchini na kuendeleza vita naye, huku Kigogo akimjibu kwa kusema kuwa yeye Zitto hatokaa hata ashike nafasi ya udiwani wa kata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Gazeti la HabariLeo liliwasiliana na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime ili kufahamu ni kwa kiasi gani jeshi linaweza kushirikiana na Zitto, kumpata huyo Kigogo, ambapo alimtaka Zitto kuwasilisha taarifa alizonazo katika Kituo cha Polisi.
Misime alisema milango ya Jeshi la Polisi, ipo wazi siku zote kufanya kazi na raia mwenye taarifa za uhalifu au mhalifu, hivyo Zitto anachopaswa kufanya ni kuziwasilisha Polisi taarifa alizonazo za Kigogo, badala ya kukimbilia kwenye mitandao ya kijamii.
“Jeshi la Polisi miaka yote imefungua milango kwa wananchi kuleta taarifa kuhusiana na matukio au watu wanaofanya uhalifu, hivyo Zitto anapaswa kuziwasilisha taarifa katika kituo chochote cha Polisi hasa ikizingatiwa kuwa taarifa alizonazo ni muhimu,” alisema Misime.
Aliongeza, “Ifahamike kama mtu akiwa na taarifa za uhalifu au mhalifu lakini akashindwa kuziwasilisha Polisi, anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria.”