Polisi yamtaka Zitto Kabwe kuwasilisha taarifa za Kigogo ili akamatwe

Status
Not open for further replies.
Hizo zingine Ni ishu ambazo hazina maana,,Ni muhimu Sana tumuweke mbaroni kigogo
Kwa kosa gani?

Anzeni na wale waliojiapiza kumuua Zitto Kabwe.
Au Musiba anayetishia maisha ya watu kila uchwao.
Au KM uchwara Bashiru anayeropokaropoka hovyo eti CCM itashinda kwa mtutu wa bunduki!

Nyie ndiyo mnaopenda kuiona nchi yetu ijitumbukize kwenye civil unrest nyie!!
 
Guy nikitaka kwenda los angel nipande gari za ubungo maziwa halafu nipande bodaboda zinazo elekea wapi tena?
 
Serikali iachane na mambo ya kipuuzi, ijikite ktk kushughulikia mambo muhimu kama ukosefu wa ajira, wanafunzi kukosa mikopo, huduma duni za afya na wajue Corona iko njiani.

Elimu inayoporomoka kila uchao, asilimia kubwa ya watanzania hawana maji safi na salama na kuporomoka kwa haki za binadamu.

Hayo ndio mambo muhimu ya kushughulikia, kumtafuta sijui Kigogo hakuwezi kutatua chochote kati ya hayo ni kufanya serikali ionekane haijui ni kwa nini iko madarakani.
 
Hawa polisi vipi mbona mikutano ya chadema huwa wanazuia kwa kusema wamepata taarifa za kiinteligensia sasa hizi za kigogo hawana?!
 
Picha
Jeshi la Polisi nchini limemtaka Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto kuwasilisha taarifa haraka za mhalifu kwa njia ya mtandao, anayetafutwa na serikali kwa muda mrefu anayejiita Kigogo, ili mhalifu huyo akamatwe.

Limesema hivyo kutokana na taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Zitto kuwa anazo taarifa muhimu zinazoweza kusaidia kukamatwa kwa mtu huyo anayejiita Kigogo.

Kwa muda mrefu kumekuwa na akaunti ya mtandao wa kijamii wa Twitter, inayotumia jina la Kigogo na sura ya mwanamuziki wa Hip Hop kutoka Marekani, Jay Z.

Akaunti hiyo hutoa tuhuma mbalimbali kwa serikali na kukosoa mara kwa mara mambo yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Hatua hiyo imekuwa ikichukuliwa ni uhalifu, hasa kutokana na shutuma nzito anazozitoa ‘Kigogo’ huyo kwa Serikali ya Rais John Magufuli.

Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola aliwahi kutoa tamko kupitia vyombo vya habari kuwa Kigogo huyo anakaribia kukamatwa.

Wiki iliyopita, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini katika akaunti yake ya Twitter, aliweka sura ya mtu aliyemtambulisha kwa jina la Didier Abdallah Mlawa anayeishi Uingereza, huku akisisitiza kuwa mtu huyo ndiye anamiliki akaunti hiyo ya Kigogo, inayoichafua serikali.

Hatua ya Zitto kufikia uamuzi huo, imetokana na wawili hao kutofautiana, ambapo katika majibizano yao, Zitto alibainisha kuwa Kigogo kwa sasa amekuwa akitaka kukabiliana na yeye, kwa kuwa ni pingamizi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku Zitto akijinadi kuwa hawezi kulaza damu katika kukabiliana na mtu kama Kigogo.

Zitto alifikia hatua ya kumtaka Kigogo, arejee nchini na kuendeleza vita naye, huku Kigogo akimjibu kwa kusema kuwa yeye Zitto hatokaa hata ashike nafasi ya udiwani wa kata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Gazeti la HabariLeo liliwasiliana na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime ili kufahamu ni kwa kiasi gani jeshi linaweza kushirikiana na Zitto, kumpata huyo Kigogo, ambapo alimtaka Zitto kuwasilisha taarifa alizonazo katika Kituo cha Polisi.

Misime alisema milango ya Jeshi la Polisi, ipo wazi siku zote kufanya kazi na raia mwenye taarifa za uhalifu au mhalifu, hivyo Zitto anachopaswa kufanya ni kuziwasilisha Polisi taarifa alizonazo za Kigogo, badala ya kukimbilia kwenye mitandao ya kijamii.

“Jeshi la Polisi miaka yote imefungua milango kwa wananchi kuleta taarifa kuhusiana na matukio au watu wanaofanya uhalifu, hivyo Zitto anapaswa kuziwasilisha taarifa katika kituo chochote cha Polisi hasa ikizingatiwa kuwa taarifa alizonazo ni muhimu,” alisema Misime.

Aliongeza, “Ifahamike kama mtu akiwa na taarifa za uhalifu au mhalifu lakini akashindwa kuziwasilisha Polisi, anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria.”
Sawa anatakiwa asaidie. Cyber crime unit mmeshindwa?
 
Naomba polisi waanze na kuwakamata wale vijana wa CCM waliofanya fujo kwenye mkutano wa Mheshimiwa Mbowe, ambao picha na majina yao yamewekwa hadharani kwenye mitandao.
 
Kigogo ni muhimu kulindwa zaidi hata ya baraza zima la wanaojiita mawaziri!
 
For me huyu kigogo hahitaji ulinzi wowote!!practically ni ngumu sana kumpata kigogo labda ajitaje mwenyewe kama Mange au wampate kwa uchawi? ngoja nisaidie wasiojua

Kigogo akiwa yuko nje ya nchi ili wampate ni lazima waongee na Twitter wapewe email address yake then waende google au yahoo au hotmail ili wapewe namba ya cm aliyoitumia kusajili email akaunti aliyotumia kujiunga twitter au IP address ambayo yaweza pia kuwa na watumiaji wengi kama anarusha makombora kwa wifi ya ofisi, ( hili la kupewa data za mhusika litafanyika siku Yesu akirudi sababu hakuna huo utaratibu wa hizo kampuni za kizungu kuvunja mkataba wa kujiunga wa wateja wake, never on earth! )

kisha labda wakipata hiyo namba ya cm waangalie ni nchi gani yupo wawasiliane na kampuni ya cm ya hiyo nchi na serikali ya nchi hiyo wapewe utambulisho na anaweza kukana siyeye anaeandika sababu ni lazima aonekane akiandika ili ahukumiwe na pia namba ya cm huhama umiliki kutoka mtu mmoja na mwingine sababu ukiacha kutumia namba anapewa mwingine!! sasa hata wakipata namba wanaweza kukuta anaetumia ni bibi wa kizungu!! kwa ulaya na US serikali yetu kupewa hiyo namba hilo litawezekana kwa kumfufua Mandela aje atoe majibu).

ningeishauri serikali yangu kuachana na wazo hilo la kumjua kigogo na badala yake kuweka kikosi cha kupambana na uzushi wa kigogo na si kigogo mwenyewe for me it is a waste of time!!

kwa wanaoishi ulaya na Us watanielewa 100% wengine am sorry!!
 
Sijaona huo "uzushi" bali ni "facts tupu" Hii ni mtazamo wangu tu! Tunapigwa sana ktk awamu hii!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom