Polisi yamtaka Zitto Kabwe kuwasilisha taarifa za Kigogo ili akamatwe

Status
Not open for further replies.

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Jeshi la Polisi nchini limemtaka Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto kuwasilisha taarifa haraka za mhalifu kwa njia ya mtandao, anayetafutwa na serikali kwa muda mrefu anayejiita Kigogo, ili mhalifu huyo akamatwe.

Limesema hivyo kutokana na taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Zitto kuwa anazo taarifa muhimu zinazoweza kusaidia kukamatwa kwa mtu huyo anayejiita Kigogo.

Kwa muda mrefu kumekuwa na akaunti ya mtandao wa kijamii wa Twitter, inayotumia jina la Kigogo na sura ya mwanamuziki wa Hip Hop kutoka Marekani, Jay Z.

Akaunti hiyo hutoa tuhuma mbalimbali kwa serikali na kukosoa mara kwa mara mambo yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Hatua hiyo imekuwa ikichukuliwa ni uhalifu, hasa kutokana na shutuma nzito anazozitoa β€˜Kigogo’ huyo kwa Serikali ya Rais John Magufuli.

Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola aliwahi kutoa tamko kupitia vyombo vya habari kuwa Kigogo huyo anakaribia kukamatwa.

Wiki iliyopita, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini katika akaunti yake ya Twitter, aliweka sura ya mtu aliyemtambulisha kwa jina la Didier Abdallah Mlawa anayeishi Uingereza, huku akisisitiza kuwa mtu huyo ndiye anamiliki akaunti hiyo ya Kigogo, inayoichafua serikali.

Hatua ya Zitto kufikia uamuzi huo, imetokana na wawili hao kutofautiana, ambapo katika majibizano yao, Zitto alibainisha kuwa Kigogo kwa sasa amekuwa akitaka kukabiliana na yeye, kwa kuwa ni pingamizi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku Zitto akijinadi kuwa hawezi kulaza damu katika kukabiliana na mtu kama Kigogo.

Zitto alifikia hatua ya kumtaka Kigogo, arejee nchini na kuendeleza vita naye, huku Kigogo akimjibu kwa kusema kuwa yeye Zitto hatokaa hata ashike nafasi ya udiwani wa kata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Gazeti la HabariLeo liliwasiliana na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime ili kufahamu ni kwa kiasi gani jeshi linaweza kushirikiana na Zitto, kumpata huyo Kigogo, ambapo alimtaka Zitto kuwasilisha taarifa alizonazo katika Kituo cha Polisi.

Misime alisema milango ya Jeshi la Polisi, ipo wazi siku zote kufanya kazi na raia mwenye taarifa za uhalifu au mhalifu, hivyo Zitto anachopaswa kufanya ni kuziwasilisha Polisi taarifa alizonazo za Kigogo, badala ya kukimbilia kwenye mitandao ya kijamii.

β€œJeshi la Polisi miaka yote imefungua milango kwa wananchi kuleta taarifa kuhusiana na matukio au watu wanaofanya uhalifu, hivyo Zitto anapaswa kuziwasilisha taarifa katika kituo chochote cha Polisi hasa ikizingatiwa kuwa taarifa alizonazo ni muhimu,” alisema Misime.

Aliongeza, β€œIfahamike kama mtu akiwa na taarifa za uhalifu au mhalifu lakini akashindwa kuziwasilisha Polisi, anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria.”
 
Wamtafute wao wenyewe. Zitto hajamripoti Kigogo Polisi hadi Polisi imuulizie taarifa zake kwake.
 
Mbona haina haja ya kua na akili nyingi sana ukiangalia tu profile picha ya kigogo unajua kabisa kigogo2014 ni shawn carter
 
Kwani wao kazi yao nini? au network za intelejensia yao zinanasa tu wapinzani na mikutano yao, huko kwingine zinaonesha chenga chenga?
Na kudukua mawasiliano ya watu wanaotongozana kwenye simu
 
Kigogo hata Mimi natamani kumjua
 
Yaani wanarespond kwa account fake?,
Yaani wanafanyia kazi majungu ya mitandaoni?.
Kuna kipindi nilimaliza la Saba,nikataka kwenda depo ,Moyo ukasita,saa hizi ningekua hata kamanda wa mkoa fulani,,,yaani najuta.
Nimeishia kuwa korokoloni kwenye hi mashine ya kusaga mahindi
 
kwani huyo Kigogo kamuua nani?

vipi assassins wa Aquiline mbona mmeweka mpira kwapani?

au wale waliomtwanga Lissu risasi 30 ....mmefikia wapi?
Hizo zingine Ni ishu ambazo hazina maana,,Ni muhimu Sana tumuweke mbaroni kigogo
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…