Polisi yasema inamshikilia msaidizi wa Membe Jerome Luanda, anatuhumiwa kwa kosa la kutakatisha fedha

Hivi unaweza kumteka mtu airport wakati anarudi na tajiri wake? Twambie mkuu alitekwa vipi? Je, Membe alijuaje ametekwa? Wanaotekwa huwa hawatoi taarifa, Je Membe alisafiri naye nje ya nchi? Kama alisafiri naye kwa nini hawakuondoka pamoja walipowasili Airport?
 
Kabla Membe hajaweka mkwara ulijua alitekwa na polisi?
Polisi wamemkamata, hawajamteka, hivyo hakuwahi kutekwa na Polisi.

Hakuna sehemu ambayo Membe ameonesha kwamba Polisi wamevunja sheria katika kumkamata huyu mtu.

Na in any case, mimi kujua au kutojua kuna umuhimu gani?

Membe na serikali ya Tanzania wanajuana madudu yao waliyofanyiana miaka kibao, sasa mimi leo itanisaidia nini kujifanya nayajua ma beef yao zaidi yao?

Waswahili walisema "Ndugu wakigombana, shika jembe ukalime. Wakipatana, shika kapu ukavune".

Watu wa upinzani waliwashobokea sana Shibuda, Lowassa na Sumaye.

Sasa hawa wako wapi leo?

Na wewe unajuaje kwamba baada ya Membe kushindwa uchaguzi hatarudi huko alikotoka kama kina Lowassa na Sumaye?

Unaelewa kwamba Membe kahama chama kwa sababu ya kutafuta urais tu? CCM ingempitisha awe mgombea urais asingehama?

Sasa wewe unapinga CCM au unapinga mtu?

Unapinga mfumoau unampinga mtu tu?

Unaelewa huu mchezo unaitwa "Membe and ACT Wazalendo: A Marriage of Convenience"?
 
Msimu wa siasa za uchaguzi huu, hata mtu anayekamatwa na Polisi anatajwa kwamba "katekwa" ili watu wapate mtaji wa kisiasa.

Mimi siwafagilii Polisi wa Bongo, wana matatizo mengi sana.

Lakini Membe naye kazidi mikwala mbuzi na cheap politics.
 
Reactions: Dua
Polisi ni watekaji, au watekaji ni polisi... kama ni kushikiliwa kwa mahojiano iweje achukuliwe bila familia kujuzwa!
Unatakiwa uelewe, amekamatwa airport nadhani alikuwa anatoka ng'ambo, polisi hawawajibiki kutoa taarifa kwa familia wanapomkamata mtuhumiwa, familia ya mtuhumiwa ndo inawajibika kufatilia taarifa za ndugu yao katika vituo vya polisi.
 
Mambosasa alikua mkuu wa kituo mererani,elimu ndogo anayo sijui nani kambeba ya kumpa kanda maalum
 
Mimi simshobokei Membe, ni wewe unayetaka kunitia kauli kinywani, kama mtu amekatwa na polisi inakuwaje isijulikane kawekwa kituo gani cha polisi?

Kwa nini isijulikane kakamatwa kwa kosa gani?

Sheria inataka afikishwe mahakamani baada ya masaa 24,je wewe umesikia kama amepelekwa mahakamani?

Kwa nini ijulikane kuwa ametekwa (amekamatwa kwa mujibu wa Mambosasa) baada ya Membe kutangaza?

Wewe labda ndio unajua kama kuna beef ya Membe na serikali yake, ni wewe unayejua kama wapinzani waliwashobokea hao uliowataja, ni wewe unayejua kuwa Membe anaweza kurudi kuunga mkono juhudi.

Mimi nachojua ni kwamba hatimaye tunaanza kuwajua wasiojulikana, taratibu za polisi za kukamata watu tunazijua mengineyo ni yenu makada wa Lumumba
 
Membe alipiga mkwala, alisema mtu wake aachiwe, akatoa mpaka masaa, lakini mpaka sasa mtu wake hajaachiwa. Membe kafanya nini?

Hilo ndilo swali langu muhimu, hayo mengine ni kimepanda kimeshuka.

Hao Polisi wa Tanzania naweza kuandika mabaya yao zaidi ya kumshika huyo mtu wa Membe.

Membe kapiga mkwala mzito mtu wake aachiliwe, tena katoa na masaa.

Mtu wake hajaachiwa.

Sasa Membe anafanya nini?

Mwanamme ukipiga mkwala halafu uonekane huwezi kufanya lolote baada ya kupiga mkwala ni kitu cha aibu.

Bora asingepiga mkwala kabisa.
 
Kabla ya Membe kuzungumza hatukujua kama polisi ndio wahusika, Kakonko Kigoma Simon Kanguye alichukuliwa na maofisa wa usalama hadi leo hajaonekana.

Azory Gwanda hadi leo hajaonekana.

Leo wamejulikana unaleta mipasho kama ulikuwa TOT na akina Hadija Kopa, tumia akili hata ya kuazima, unawajua waliomteka Roma mkatoliki?

Unawajua waliomteka MO Dewji?

Kipanya je?

Ukada unakutia uchizi, mimi sina stress hapa na enjoy picha la kihindi wewe mishipa ya shingo inakutoka, una maslahi gani binafsi? Just give me a break
 
Hata mimi Membe simkubali kabisa lakini kama huo usanii wake umeweza kumtoa nyoka pangoni na kukiri kwamba ni wao wanamshikilia na si wanaodaiwa kutojulikana, nitasifu mkwara wake bila kujali umepangwa au vipi.

Kwangu mimi, tangu kile kisa cha Tarime nilianza kuamini kuwa hawa wanaoitwa wasiojulikana ni hao hao na hata sasa naamini kama huo mkwara (feki?) usingekuwepo huyo mambo gani sijui hangejitokeza na kukiri kuwa wanaye.

Taratibu na kanuni za polisi kukamata watu zinajulikana na kama hao polisi wangezifuata nisingekuwa na neno...nje ya hapo ni kuteka, period. Wanaodaiwa kutojulikana ni hao hao wanaojitokeza mkwara (mbuzi?) unapowekwa.

Miaka yote nasema hatuna polisi, tuna genge tu la wadhulumaji na hilo genge CCM wanajua kulitumia vizuri sana kung'ang'ania madaraka yanayowazidi uwezo. Mwaka huu hata wakishinda tena wajue wananchi taratibu wanazinduka.
 
Na bado kuna wanaojitoa ufahamu na kutaka kutulazimisha na sisi tusiwe na ufahamu kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na haki za kuishi, haya mambo yasipokemewa kwa sauti kubwa yatakukuta hata wewe unayetetea ukijiona ndio kada mbobezi
 
Na bado kuna wanaojitoa ufahamu na kutaka kutulazimisha na sisi tusiwe na ufahamu kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na haki za kuishi, haya mambo yasipokemewa kwa sauti kubwa yatakukuta hata wewe unayetetea ukijiona ndio kada mbobezi
Chochote kitakachomtokea huyo msaidizi wa Membe, kila mtu atajua wahusika ni polisi na huo ndio uzuri wa kukiri kwao. Kila mtu sasa anajua polisi wananmshikilia na si jukumu la ndugu na marafiki kuhangaika kumtafuta eti kutoka kiuto kimoja cha polisi hadi kingine kama anavyodai huyo kilaza mambo sijui.

Inatakiwa ukifika kituo chochote cha polisi kuulizia aliko ndugu yako na kama ni kweli anashikiliwa na polisi inatakiwa upate majibu hapo hapo na si uzungushwe kutoka kituo kimoja hadi kingine. Huo ni utaratibu wa kishamba na wa kijinga sana kwani wana namna ya kuwasiliana na kukupa majibu stahiki.
 

Ukada wa chama gani? Mimi sina chama Tanzania. I am an equal opportunity critic.

Unarudia mule mule ambako ushaeleza nimekwambia that is irrelevant.

Membe kafanya nini?

Hatutaki rais ambaye atapiga mikwala watu maadui wa nchi yetu, halafu wakimjambisha ananywea.

Membe kafanya nini baada ya mikwala yake?
 
Kenya uganda Rwanda Burundi pesa za kigeni kuingia hawana shida hata upite na kiroba cha dola hawana Tatizo ili mradi hiyo pesa isalie hapo isitoke nje, wana sera za ingiza pesa itumike siyo kutoa pesa Nchini mwao kuzipeleka nje, kwa Tanzania ni hovyo kabsa ukileta pesa inakuwa tabu kubwa wakati pesa zinakuja kuleta maendeleo
 
Kwanza kama ishu inamuhusu jasusi ilitakiwa akamatwe yeye na sio msaidizi, wanaonea dagaa wamfate kambale waone moto..
inasemekana wamekamata wengi wanaowasiliana na membe na huyo msaidizi wa membe ni hatari kuwasiliana na membe kwa sasa
 
Wote waliokuwa wakiwasiliana na membe tokea huko alipokuwa wanachunguzwa na wengine kadhaa wamekamatwa wapo ndani
 
Yeyote aliyewasiliana na membe akiwa Dubai ajue akitua uwanja wa Ndege hapo Dsm atakamatwa,
 
Ametakatisha fedha zilikuwa chafu ? Kuzifanya ziwe safi ni Kosa Mambosasa?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…