Kabla Membe hajaweka mkwara ulijua alitekwa na polisi?
Polisi wamemkamata, hawajamteka, hivyo hakuwahi kutekwa na Polisi.
Hakuna sehemu ambayo Membe ameonesha kwamba Polisi wamevunja sheria katika kumkamata huyu mtu.
Na in any case, mimi kujua au kutojua kuna umuhimu gani?
Membe na serikali ya Tanzania wanajuana madudu yao waliyofanyiana miaka kibao, sasa mimi leo itanisaidia nini kujifanya nayajua ma beef yao zaidi yao?
Waswahili walisema "Ndugu wakigombana, shika jembe ukalime. Wakipatana, shika kapu ukavune".
Watu wa upinzani waliwashobokea sana Shibuda, Lowassa na Sumaye.
Sasa hawa wako wapi leo?
Na wewe unajuaje kwamba baada ya Membe kushindwa uchaguzi hatarudi huko alikotoka kama kina Lowassa na Sumaye?
Unaelewa kwamba Membe kahama chama kwa sababu ya kutafuta urais tu? CCM ingempitisha awe mgombea urais asingehama?
Sasa wewe unapinga CCM au unapinga mtu?
Unapinga mfumoau unampinga mtu tu?
Unaelewa huu mchezo unaitwa "Membe and ACT Wazalendo: A Marriage of Convenience"?