Polisi yavamia kikao cha ndani cha CHADEMA jimbo la Segerea, Patrick Asenga na wenzake wakamatwa

Hii nchi Jeshi la Polisi linatumika vibaya na miccm, ubwa wakubwa nyie
Si wewe ulikuwa unausifia utawala huu? Yapo wapi sasa ila tuliwaonya mkatuona mahayawani
 
Tatizo la CHADEMA ya sasa ni ugaidi. CHADEMA kiliondoka na Dr. Slaa
 
Kwa haya yanayo tokea wana ccm amkeni maana shimo unalo mchimbia mwenzio na ww kuna siku watakuchimbia ni swala la mda tu .Watu mnao furahi kuona chadema wao hawana haki ya kufanya mikutano wakati ccm wanafanya siku mambo yakibadilika napo mshangilie.Hii nchi yetu sote tuipende na tupendane kwani hao chadema wakifanya mikutano tunapungukiwa nn si hasira zao zinapungua lakini mkiwanyima haki hata ya kuongea ndo tunapalia mkaa amani ya nchi kutoweka.
 
Tuna Polisi wakipuuzi mno
Harakati bambikabambika,hapo sijui watapata wangapi wakubambikia kama mwenye kigoda.Sio kwa kuogopa huko dai pendwa la wananchi la katiba mpya.
 
Hebu nitafutie post hata moja nikisifia, nitafutie post moja tu tangu 2008
Umesahau ulivyokuwa unamponda JPM na alipoingia Samia ukademka kweli na sasa niwape pole tu maana niliwaambia hapa JF. Nakuletea uzi
 
Ili polisi apandishwe cheo au aongezewe marupurupu ni lazima apambane na chadema kwanza
Ni kama huko kwenu chadema ili uaminike kuwa ni kamanda lazima upambane na kuwachokoza polisi
 
Wakamateni wote. Mkiwamaliza basi serikali iongoze nchi ya maaskari Tu bila familia zingine.
 
Mungu ibariki CHADEMA
 
Kama inavyo semekana Mbowe alikuwa anaajiri/recruits askari na wanajeshi waasi kwa lengo la kuhujumu serikali na kuuwa viongozi wa serikali, basi kwakweli Mbowe alifika pabaya sana, siajabu ange ajiri hata wahamiaji haramu kwa lengo baya zaidi.
Matendo haya hayana tofauti na yale wanayo yafanya Bokoharam.
hata hivyo Jeshi la Polisi wakishirikiana na vyombo vyote vifanye upelelezi wa kina na kwa weledi wa viwango vya juu.
 
Ndugu,
Hivi si mlishasema na kusemaga kuwa CHADEMA iliishajifia? Wengine wanaimba hadharani na kudai kilikwisha zikwa.
Vipi tena mwaonekana kuhangaika namna hii kama kuku anaetafuta pa kutaga?
Wajameni kama huko ndio mwaita kuupiga mwingi basi mtafika hafutaimu mkiwa mwatambaa.
 
TWASUBIRI hili kama tunavyosubiri ushahidi utakaotolewa mbinguni na Madelu.
 
huyo namba 8 alikuwa sisiemu damu,damu
hivyo kuweni makini na wapelelezi ndani ya vikao
msipoangalia hata kikao kifanyike pangoni mtakamatwa.
 
chadema kwa ilipofika imekua kama imani...na watu wakiamini hata mitutu ya bunduki haiwezi kufanya watu waikane imani yao. Naona anguko la mbogamboga.
 
mama ushungi kachachamaa na chadema .. asijisahau 2025 ni karibu tu hapo watakuja kumfunua
 
Mzimu wa mwendazake ndio unaongoza awamu hii kama roboti.Naona shujaa wa Africa anatuongoza kiroho kupitia mzimu wake
 
Police wanazidiwa weledi hata na police wa nchi ndogo tu kama malawi huwezi kuta wanasaidia chama tawala kujibu hoja za wapinzani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…