Polisi yavamia kikao cha ndani cha CHADEMA jimbo la Segerea, Patrick Asenga na wenzake wakamatwa

nilishakufahamu kitambo sana , hilo ulijue , hatuingii mitandaoni kibwege
Bado hujajibu hoja ya nyie kususa kila jambo. Hata la kuomba dhamana mnapokamatwa na polisi nalo mlishasusa. Maandamano ya barabarani kama ilivyokuwa kawaida yenu huko nyuma, mlishasusa singu nyingi. Hata haya maandamano yenu ya kwenye mitandao ya kijami kama Jf yanakaribia mwisho, wengi wenu wameshayasusa. Mmebaki watu msiozidi 10.
 
Ukiona mtu anatukana katika mijadala, jua ameishiwa na hoja na ni wa kuogopwa kama ukoma
Hahahahaha samahani sikua na maana mbaya, nilikasirika kidogo baada ya kuendelea kunihusisha na CCM. My apology
 
Udikteta unazidi kupamba moto Tanzania.
 
Hivi wewe hujiulizi tu mbona NCCR hawana vurugu??

Najua jibu utakalokuja nalo ni NCCR sio wapinzani.

Ila serious mkuu, jiulize why kila siku CDM??
Siwezi kusema hayo,maana nawafahamu NCCR Mageuzi ni wapinzani.Nao pia waliwahi kupata mateso kama wanayopitia CHADEMA kipindi kikiwa na nguvu zake enzi za Agustin Mrema.CCM waliwatenda maovu hadi wakatepeta na Mh.Mrema akawakimbia ndipo walipokosa zile nguvu zao asilia.Ila bado wapo vizuri kwenye hoja na wanaenda vizuri Bali siyo tishio kwa CCM kama ilivyo CHADEMA leo.
Kula Siku CHADEMA kwa sababu they are consistent and threat to CCM pamoja na vituko vyote walivyofanyiwa.Hoja zao ni mwiba mchungu kwa watawala chini ya Mwenyekiti asiyetetereka Kamanda Mbowe.Hilo kwa CCM ni kosa lisilovumilika na wanawatumia POLISI na Mahakama kuwafifisha na kuwatisha.
Tuendelee kupaza sauti tupate Katiba ya Wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…