Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar kupitia Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, ilikuwa inafanya Uchunguzi wa Shauri la KUJARIBU KUJINYONGA linalomhusu Raia wa Kigeni ajulikanae kwa jina la ASHLEY JENNAE ROBINSON, Raia wa Marekani, mwenye umri wa miaka 31. Tukio lililotokea tarehe 08/04/2026 majira ya saa 20:55hrs katika hoteli ya ZURI iliyopo NUNGWI, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Marehemu ASHLEY JENNAE ROBINSON, aliingia hoteli ya ZURI tarehe 06/04/2026 akiwa na mchumba wake aitwae JOSEPH ISAACK MCCANN na kupangishwa Nyumba/Villa namba 25.
Siku ya tukio, tarehe 08/04/2026 majira ya saa 12 jioni kulitokea hali ya kutokuelewana baina ya marehemu na mchumba wake, ambapo walikuwa na mizozo isiyoeleweka ina muktadha gani.
Taarifa ya kutokuelewana kwao ilifika kwa Uongozi wa hoteli, Uongozi wa hoteli uliamua kumhamisha mchumba wake na kumpangia Nyumba/Villa namba 65 kwa muda wakati suala lao la kutoelewana likiendelea kushughulikiwa na Uongozi wa hoteli ambapo marehemu ASHLEY JENNAE ROBINSON alibaki kwenye Nyumba/villa namba 25.
Soma Pia:

- Polisi inamshikilia Joe McCann, Mchumba wa marehemu Ashly Robinson maarufu kama "Ashlee kwa mahojiano
- Polisi: Mwanamtandao Ashlee Jenae alifia Hospitali baada ya kukutwa amejinyonga