Poll: Is it time for Raila Odinga to retire from active politics?

Is it time for Raila Odinga to retire?

  • Yes

    Votes: 25 69.4%
  • No

    Votes: 11 30.6%

  • Total voters
    36

Unaonekana kuzijua siasa za Kenya ila kuna maeneo unafaa kurekebishwa wewe mtu wa Zitto Kabwe, au labda wewe Zitto unatuzuga tu humu.

Sasa naomba nikuweke sawa, itakua rahisi kwanza nikupe historia kidogo kuhusu matokeo ya 2013, Jubilee ilitimiza magavana 18 ilhali wa mlengo wa CORD walifikia 23

Sasa leo hii Jubilee wameongeza kutoka kwa hao wa awali 18 hadi 25 na isitoshe wamewapata kutoka kwenye ngome za NASA. Hicho ni kipigo, kwanza ukihesabu wabunge na maseneta yaani hadi wengine wetu tunaanza kuwa na wasiwasi maana upinzani umevunjwa vunjwa kiasi cha kuachia serikali, halafu uongeze kwamba Raila kuna uwezekano mkubwa akastaafu maana tulimtegemea kwenye kupiga mayowe kila wakati uozo ukichipuka.
 
una point mkuu Raila is influential ila sasa siasa za Afrika kukumbalika mijini kuliko vijijini kwa upinzani ni kawaida nadhani sababu ni nyingi...ila sasa karibia ngome zote za Raila Uhuru amepenya ndugu meaning walivyotegemea Nasa walichemka tazama Western kwa Mudavadi walijua watazoa kura zote matokeo yake wamegawana na Uhuru...huu uchaguzi umetoa picha mpya Kenya kwamba kumbe ukabila wakiweka pembeni wanaweza kupigakura bila kwa ushawishi wa sera....Raila kwa sasa aede mahakamani akawakilishe kesi na kama ushahidi upo wa kutosha basi mahakama itaamua nini kifanyike...vinginevyo kutegemea watu wachapana ndio aingie serikalini amechemka ukizingatia sio miji yote hio unayodai mikubwa imemsapoti...yeye ni Nairobi,Kisumu na Mombasa...hapo watadhibitiwa tu Matiang'i sio waziri wa mchezo
 
Hahahahahaa ngome mmewapiga??? Ngome gani hiyo mkuu niambie hata moja ambayo jubilee kaitoa kwa NASA zaidi kidero tu ambaye mlishinda kwa gap ya 100,000 thousand votes pekee hivyo sio significant gap kutuaminisha kuwa NASA stronghold was overrun mfano mombasa mlimuweka kibaraka wenu omar hassan ameaibika!! Machakos kitui mbona hamjazirudishi jubilee ilihali kulikuwa na internal wiper conflicts???

Hao jubilee mbona wametolewa huko bungoma na kina wafula??? Au hiyo hukuiona kwa ufupi jubilee had the government by now it was supposed to have a moderate advantage of above 65% ya senate na gubernatorial seats sio mnagawana nusu na other parties kwa ufupi ni kwamba jubilee imekataliwa kwenye nusu ya kaunti za kenya because if u have a government for 5 years and still fail to win half of nation's counties it means simpy UMEKATALIWA na wakenya unlike for odinga and NASA who had nothin to lose afterall they had no NASA/CORD government for the last 5 years

All in all conclusion is HALF OF KENYA HAIMTAKI JUBILEE/UHURU.....
 
Hahahahahaa mombasa na nairobi!!!! Hivi unajua hta turkana ana support?? Ukambani huko machakos na kitui umehesabau?? Coast yote je kuaanzia kilifi mpaka malindi huko mombasa kote ni odinga tu kumbuka hata kwa waluhya huko sijui vihiga mpaka busia huko kote ODM tupu!! Mkuu dont underestimate Raila kumbuka ana 7 milion votes!!! Its not easy kufikisha hizo kura against an incumbent ambaye kwenye kila kampeni alizindua kwanza mradi wa mabilion!!!

Huyo matiang'i hana lolote kma wakenya wakiamua alikuwepo Moi baba wa siasa ila wakenya walipoamua mbona alibaki kma sanamu la mmakonde tu!!!!

Kwa ufupi ni hivi jubilee haikubaliki no wonder kwenye county 47 imeambulia 24 pekee yaani 51% meaning 49% hawamtaki uhuru upo hapo!!!
 

Nafikiri mahesabu ya siasa utakua huyajui vizuri, kila serikali hupoteza sana kwenye kugombea muhula wa pili, nakushangaa ukisema Uhuru alifaa kuwa na zaid ya asilimia 65%. Ukifuata historia ya Kenya, marais wote hushuka umaarufu kadiri wanavyozidi kuwa kwenye madaraka.
Uhuru amefaulu kuongeza asilimia zaidi ya aliyokua nayo kwenye muhula wa kwanza.

Halafu sielewi kile unachong'ang'ania kwenye idadi ya magavana, kumbuka gatuzi nilizoziorodhesha hapa chini hazikua za Jubilee, wamefaulu kuzichukua

GARISSA
KAJIADO
KWALE
LAMU
MARSABIT
NAIROBI
WAJIR
 
Mkuu mbona pia huongelei ambazo jubilee ameangushwa???? Kwa ufupi nimesema jubilee wana 51% majority ya kaunti meaning half of the counties hazimtaki jubilee na uhuru wake ilihali alikuwa na serikali while upinzani haukuwa serikalini!!! Upo hapo???

Pia two wrongs dont make a right eti kwakuwa alikuwa serikalini basi ndio huwa umaarufu unashuka so ndio inajustify uhuru kushuka umaarufu??? Hiyo sio hoja ya msingi kabisa mkuu the thing is odinga had nothin to lose so to gain 7 million votes is a serious message kuwa uhuru hakubaliki kabisa though anajisifia kuwa amefanya maendeleo sana ....
 
Kwa Watanzania wanao sema Odinga kashidwa kwa sababu ya urafiki wake na Magufuli mnakuwa wavivu kufikiri. Odinga ni mwanasiasa mkonge, isingekuja kutokea hata siku moja akaacha washauri wake wa ndani eti amsikilize Magufuli, au Magufuli na yeye akacha washauri wake amsikilize Odinga. Wapiga kura wa kenya walipiga kura kutokana na shida zao za ndani ya nchi na wala sio kwasababu fulani ana rafiki wa fulani.
 
Mkuu ukweli huu watu hawauelewi tunabaki kumzodoa Raila bila kuangalia chanzo cha kuanguka kwake!!

Ninachojua mambo wanayofaidi leo wa Kenya ni matunda ya kazi ya Raila eg Katiba mpya, Tume huru na hata teknolojia ya uendeshaji wa chaguzi hizi zote ni matunda ya kazi yake. Bahati mbaya Africa haijawa tayari kwa democracy

Cairo's
 
Hivi hiyo mikoa uliyoitaja japo juu ni yakujivunia kweli? Hebu weka idadi yawapiga kura wa maeneo hayo au wanachi waoishi huko.

Muhula wa pili ni kipimo cha muhula wa kwanza. 51% ya Jubilee ni kama unfinished business. Sio safe kufanya maamuzi yoyote ya kidemokrasia, shida inakuja pale baadhi ya wana Jubilee wakiamua kushirikiana na NASA katika mijadala ambyo hawapezani na maamuzi ya Jubilee.
 

- Jubilee hawajapoteza kiti chochote cha ugavana kwenda kwa NASA, kuna viti viwili tu ambavyo vimechukuliwa na wagombea binafsi waliokua wanaegemea upande wa Jubilee
- Kiti cha Bungoma unachotaja taja humu hakikua cha Jubilee, ni kwamba gavana aliyekuwepo awali aliamua kukitetea kwa kutumia Jubilee
- Nimekutajia kwamba umaarufu wa Uhuru umeongezeka ukilinganisha na asilimia alizoshinda nazo kwenye uchaguzi wa 2013, kwanza 2017 hawa jamaa wa upinzani waliungana wote dhidi yake
- Pia nimekuambia ni kawaida kwa rais kupunguza umaarrufu wakati anatetea kiti kwa mara ya pili, lakini hilo halikutendeka kwa Uhuru
- Hesabu za chekechea ni kwamba mwaka wa 2013 Uhuru aliibuka na magavana 18, mwaka huu amezoa 25
 

Hizo ni gatuzi mpya ambazo hawakua nazo, humo kuna Nairobi yenye wapiga kura 2,304,386, Kajiado yenye 409,266 sasa sielewi unakusudia nini.
Kumbuka 2013 walikua na gatuzi 18 sasa wanazo 25
 
Hizo ni gatuzi mpya ambazo hawakua nazo, humo kuna Nairobi yenye wapiga kura 2,304,386, Kajiado yenye 409,266 sasa sielewi unakusudia nini.
Kumbuka 2013 walikua na gatuzi 18 sasa wanazo 25
Gatuzi muhimu hapo ni Nairobi tuu, zingine za huko kaskazini na za mashariki ni za kujazia tuu. Miaka mitano ijayo haitakuwa myepesi kwa Jubilee kama wakitaka kuleta mabadiliko makuwa kupitia njia ya kidemokrasia. Labda kama watakuwa wanapitisha kwa maamuzi ya bwana mkubwa (executive orders).
 
Hizo ni gatuzi mpya ambazo hawakua nazo, humo kuna Nairobi yenye wapiga kura 2,304,386, Kajiado yenye 409,266 sasa sielewi unakusudia nini.
Kumbuka 2013 walikua na gatuzi 18 sasa wanazo 25
Mkuu unahesabu nairobi ambayo mmeshinda kwa gap ya kura laki 1??? Unasahau kina shebesh wameachwa kwa kura zaidi ya laki 2 na passaris ??? Huku ODM wakiwa na wabunge kibao hapo nairobi???

Mkuu NASA wana mombasa na kisumu ambapo wapiga kura wake ni wengi kuliko hizo kaunti alizoshinda jubilee
 

Sikuelewi unatumia mantiki ipi maana nimesema walikua na gatuzi 18 muhula wa kwanza, sasa zimeongezeka na kuwa 25, hapo sijahesabu gatuzi ambazo zilinyakuliwa na magavana walioegemea upande wa Jubilee. Likija kwa wabunge ndio usipime, yaani Uhuru raundi hii ashindwe mwenyewe maana Wakenya wamemkubali na kumpa kura vilivyo, ana dhamana kamili, atimize miradi aliyoanzisha.
 
Sawa hawajapoteza ila je serikali kuambulia 51% pekee ya kaunti ndio inareflect claims zako kuwa jubilee imeongezeka ushawishi??

2. Hamna shida kma hakuwa jubilee ila as long as alipigiwa kampeni na uhuru na bado aliangukia pua then inaonyesha kuwa jubilee haikubaliki maana incumbent + support ya rais unaangukaje???

3 umaarufu umeongezeka wakati umemuacha mpinzani kwa kura 1 million?? Yaani five year ndio anaongezeka only 500,000 votes pekee?? Ndio popularity??? Duh its a big joke

4.ni kawaida rais kupungua umaarufu? Ndio nasema two wrongs make a right?? Yaani kisa its a trend basi kenyatta naye akishuka umaarufu ni sawa tu??? Yaani una boastbue popular while 7 million people rejected you??? Yaani half ya nchi haikutaki ndio unasema its normal??

5. Mkuu usizunguke ukweli ni kwamba ana kaunti 24 out of 47!!!! Ndio popular huyo??? Hahahahahahahaha
 

Kaka Nairobi Jubilee wameifagia
- Kati ya maeneo bunge 17 wamzeoa 9, kuna maeneo hawakua nayo wamefaulu kuongeza
- Wamechukua ugavana ambao haukua kwenye mikono yao
- Wamedumisha Useneta
- Wakapoteza Mwakilishi wa kina mama ambaye huyo Passaris amepewa kura nyingi na watu wa Jubilee waliompenda
 

- Narudia tena, Kenyatta hajapunguza umaarufu, ila ameongeza ambapo ni tofauti na ilivyo kawaida Kenya.
- Sio kila gavana aliyepigiwa debe na rais aliibuka kuwa mshindi, ni jambo la kawaida hilo, kumbuka kuna hata magavana wa kujitegemea waliofaulu kushinda wale wa rais. Japo tu wanaegemea upande wake
- Mnamo 2013 Uhuru alishinda kwa 51%, leo hii ameshinda kwa 54% wakati upinzani wameungana wote na kukusanya kura zao
- Kenya huwa kuna ushindani balaa, kwa rais kuzoa 54% sio mchezo, yaani hapo jamaa aliuza sera zake mpaka basi.
 
Kazi kweli kweli naona hapa tunaweza kesha kudebate obvious things yaani unasema maeneo bunge 17 then chama chenye serikali kiu kinaambulia 53% ya majimbo ya nairobi its an achievement????

Unadai passaris alipewa na jubilee je odinga kura zote zile za nairobi alipewa na nani??? Kidero je kura zote zile malaki alipewa na nani???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…