Brooklyn, upinzani gani Dodoma?, samahani wana bodi, sio kuwa nataka kuleta hoja za ukabila, au umajimbo, lakini kuna baadhi ya maeneo, mwamko wa kisiasa bado ni mdogo sana, hivyo vugu vugu la upinzani liko chini sana, moja ya maeneo haya ni Dodoma na Singida, na baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kusini.
Nimefanya kautafiti kwa trend ya vuguvugu la upinzani, nikakuta ile mikoa iliokithiri kwa umasikini uliotopea, ndiko ambako huwaelewi chochote kuhusu siasa za ushindani, yoyote tuu yule atakayegawa fulana na kutoa shibe tuu japo ya siku moja kabla ya uchaguzi, huyo ndiye atakaye komba kura zote kesho yake. Dodoma ni moja ya maeneo yenye umasikini huu. Umasikini huu, haitokani na watu bali kukosekana kwa mazao ya biashara ambayo yangeinua hali za maisha ya watu. Ukiangalia wasomi wa Dodoma enzi hizo, lazima walisomeshwa na misheni vinginevyo wengelipa ada kwa fedha gani?.
Haya nimeyashuhudia Busanda, kiwango cha umasikini ni cha hali ya juu, Chadema wakafanya uhamasishaji wa hali ya juu, siku ya mwisho, wajumbe wa nyumba kumi kumi wa CCM walipeleka nusu kilo nusu kilo tuu ya sukari kwenye nyumba zao kumi kumi na kiasi kiasi cha mboga, jana yake walilalia pilau, wakaamkia kifungua kinywa hivyo wameshiba, kura wampe nani?!... na na matokeo yalibadilika.
Angalia mikoa yenye neema, Arusha, Moshi na Bukoba, walifanikiwa kutokana na kuwepo kwa zao la kahawa hivyo kuwa na fedha kusomesha watoto wao hadi kupelekea kasumba kuwa Wachagga na Wahaya wana akili sana, hapana ila tangu wazazi wao walipata hizo opportunities. maeneo haya vugu vugu la upinzani liko juu kwa sababu watu hawachukui uamuzi kufuatia shibe ya siku moja.
Kwa maeneo kama Tarime, huko ni makabila yenye msimamo usioyumba, kwa Dodoma upinzani safari bado ni ndefu, CCM itampitisha Mzee kuendelea na huyo kijana atapoozwa na ukuu wa Wilaya. Miaka mitano mingine mbona sio mbali, tatizo ni mwamko, by then mambo yaweza kuwa yameshabadilika.
NB: Hii tafiti yangu nimeifanya kwa kuangalia trend tuu, hivyo sio tafiti yakinifu yenye kufuata mising ya utafiti, no research methodoloy, I was just a 'manwatcher'