Kwetunikwetu
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 1,535
- 412
JF utawala mimi nilidhani niliwaonya sana kuhusu speculating ID za members hapa, nikadhani kwamba mmelidhibiti hilo kumbe bado lipo mpaka leo? Nyie endeleeni na huo mchezo ninaamini kwamba wengi wenu bado hamjaelewa madhara yake, tuulizeni tuwafahamishe maana kuna siku mtalia kilio cha mbwa humu mtakaporudi bongo!
FMEs!
Brooklyn, upinzani gani Dodoma?, samahani wana bodi, sio kuwa nataka kuleta hoja za ukabila, au umajimbo, lakini kuna baadhi ya maeneo, mwamko wa kisiasa bado ni mdogo sana, hivyo vugu vugu la upinzani liko chini sana, moja ya maeneo haya ni Dodoma na Singida, na baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kusini.
Nimefanya kautafiti kwa trend ya vuguvugu la upinzani, nikakuta ile mikoa iliokithiri kwa umasikini uliotopea, ndiko ambako huwaelewi chochote kuhusu siasa za ushindani, yoyote tuu yule atakayegawa fulana na kutoa shibe tuu japo ya siku moja kabla ya uchaguzi, huyo ndiye atakaye komba kura zote kesho yake. Dodoma ni moja ya maeneo yenye umasikini huu. Umasikini huu, haitokani na watu bali kukosekana kwa mazao ya biashara ambayo yangeinua hali za maisha ya watu. Ukiangalia wasomi wa Dodoma enzi hizo, lazima walisomeshwa na misheni vinginevyo wengelipa ada kwa fedha gani?.
Haya nimeyashuhudia Busanda, kiwango cha umasikini ni cha hali ya juu, Chadema wakafanya uhamasishaji wa hali ya juu, siku ya mwisho, wajumbe wa nyumba kumi kumi wa CCM walipeleka nusu kilo nusu kilo tuu ya sukari kwenye nyumba zao kumi kumi na kiasi kiasi cha mboga, jana yake walilalia pilau, wakaamkia kifungua kinywa hivyo wameshiba, kura wampe nani?!... na na matokeo yalibadilika.
Angalia mikoa yenye neema, Arusha, Moshi na Bukoba, walifanikiwa kutokana na kuwepo kwa zao la kahawa hivyo kuwa na fedha kusomesha watoto wao hadi kupelekea kasumba kuwa Wachagga na Wahaya wana akili sana, hapana ila tangu wazazi wao walipata hizo opportunities. maeneo haya vugu vugu la upinzani liko juu kwa sababu watu hawachukui uamuzi kufuatia shibe ya siku moja.
Kwa maeneo kama Tarime, huko ni makabila yenye msimamo usioyumba, kwa Dodoma upinzani safari bado ni ndefu, CCM itampitisha Mzee kuendelea na huyo kijana atapoozwa na ukuu wa Wilaya. Miaka mitano mingine mbona sio mbali, tatizo ni mwamko, by then mambo yaweza kuwa yameshabadilika.
NB: Hii tafiti yangu nimeifanya kwa kuangalia trend tuu, hivyo sio tafiti yakinifu yenye kufuata mising ya utafiti, no research methodoloy, I was just a 'manwatcher'
ikibidi HUKUMU YA KIFO kwa watoa na kupokea rushwa wakati wa uchaguzi
I trust Issa Michuzi -- As per Issa Malecela kashindwa -- Ron-- US
MZEE MALECELA AKUBALI MATOKEO
HABARI TOKA JIMBO LA MTERA LINASEMA MGOMBEA LIVINGSTONE LUSINDE AMEMSHINDA MH. JOHN SAMWEL MALECELA KATIKA KURA ZA MAONI NA ANATEGEMEA KUWA NDIYE ATAYEPITISHWA KUGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CCM KWA JIMBO HILO, KWA MUJIBU WA MATOKEO YALIYOTANGAZWA SAA 4 LEO
Mkuu haya maneno ni baada ya Mwakalinga kushindwa au?
Mkuu vipi bana! after october mwenye kuteua wabunge wa jimbo la Ikulu ni Dr, umesahau nini! tehe tehe tehe! Jamaa si apumzike tuu, maana nasikia jamaa hata mshiko anao wa kutosha.Hivi kuna aliyekuwa akicheza na ID za watu humu kama FMES hasa tuliowahi kutofatiana naye katika hoja mbalimbali humu? Tusijisahau, humu tunaandika na akina Invisible hawayafuti maandishi haya. Humu ni zaidi ya Hansard ya Bunge letu.
Turudi kwenye hoja. Mzee JSM sio mtu wa kukata tamaa na wala hii sio mara yake ya kwanza kuanguka. Atanyanyuka tu. Ikishindikana kabisa JK amkumbuke kwenye jimbo lake la IKULU endapo vikao vya juu vya CCM vitashindwa kumuengua dogo Lusinde.
FMES;
Lkn hii ya Mzee maarufu kisiasa kama Malecela kusubiri hadi kura ya mwisho ihesabiwe ndiyo atangazwe mshindi,wewe kama mtu wa karibu wa Mzee huyu hali hii unaichukuliaje kwake kisiasa?
Kama kafanya vyema kwa wapiga kura wake wa Mtera wakiwemo wana CCM wenzake why isiwe kama wenzake akina Sitta,Sendeka,Mama Kilango au Lembeli ambao mara tu baada ya"exit polls"wafuasi wao walijimwaga barabarani kushangalia ushindi wao?
Mzee Malecela kawakosea nini wana CCM-Mtera hadi wakamsulubu kiasi hiki,pengine vibaya zaidi hata kuliko ya mwaka 1985 alipoangushwa na "mzee mwenzake"fundi bomba Yohana Mazengo kwenye ubunge jimbo la Chilonwa?
Why mwanasiasa Chipukizi kama Lusinde amsumbue Mzee Tingatinga kiasi hiki?Kakosea wapi Mzee wetu Cigweyemis?
UKO na SLAA AU UKO NA MAFISADI. Nyambala, uko wapi??????
Mkuu Fmes, Posts zako zimekuwa zinaleta mwamko mkubwa wa watu kuja hapa jamvini mara kwa mara na hilo lita thihirishwa na siku za karibuni ulipokuwa haupo hapa kumekuwa na mpoozo wa aina fulani.Lusinde and the "Machine" at this point wanajaribu sana kubadili kura za kata mbili, nazo ni LOJE na CHINOBOLI ili watangaze rasmi ushindi wa dogo, lakini kuna watoto wa Malecela on the scene na hasa katika kuhesabu kura hizo who are making it difficult, bado kuna kamchezo kanaendelea what a rollercoster! Haters poleni sana, ila JF haiamui nani awe mshindi.
JF utawala mimi nilidhani niliwaonya sana kuhusu speculating ID za members hapa, nikadhani kwamba mmelidhibiti hilo kumbe bado lipo mpaka leo? Nyie endeleeni na huo mchezo ninaamini kwamba wengi wenu bado hamjaelewa madhara yake, tuulizeni tuwafahamishe maana kuna siku mtalia kilio cha mbwa humu mtakaporudi bongo!
FMEs!