Habari wana JF,
Kwa mwanamke ambaye hajawai kupata mimba kabisa,siku zake za hedhi hazina mpangilio maalumu na amegundulika kitaalamu ana Polysistic ovarian syndome(vivimbe vidogo vidogo kwenye ovaries).
Je anaweza kufanyaje ili apate mimba haraka?Hospitali wanampa dawa ila tatizo bado liko pale pale, kwa sasa anatibiwa mkoani Arusha ila anatamani sana kupata ata tiba mbadala kwa ajili ya kuweza kupata ujauzito ndoa iko mashakani.
Na pia chakula gani anaweza kula kufanya awe na uwezo mkubwa wa kuweza kupata ujauzito?
Asanteni