Ndenji five
JF-Expert Member
- Nov 1, 2021
- 1,985
- 3,109
Niende moja kwa moja kwenye mada.....
Basi miezi mitatu iliyopita nilikuwa nimechelewa kurudi nyumbani, yote sababu nilipitia sehemu kwaajili ya kupata moja baridi, nilivyofika bar nikaagiza kinywaji, nikakipiga Na kuanza kurudi home hapo ni kama saa tatu, hivi usiku nikiwa zangu kwa miguu sina hili wala lile, nafika pacha moja hivi.
Ghafula mwili wangu ukahisi hatari, nywele zikiwa zinasisimka na hapo ndipo woga ulipoanza kunitawala, nikajikuta nakimbia pasipokujua nini kinanikimbiza, cha kushangaza ile nakimbia ukapita upepo mmoja hivi mkali, nikajikuta nipo kwenye kundi la watu huku nimebebwa juu juu na watu kama wa nne hivi, ni warefu, kama futi 30 hivi kupanda hewani, rangi zao ni kijani wengine ni wekundu, basi ikawa napelekwa kwenye chumba maalumu na kufungiwa humo, nikiwa nimeketi katika lijumba hilo, akatokea mbwa akatoa ishara kama ya kuniuliza kitu kwa lugha ya kishetani, ninavyosema ya kishetani naweza nisieleweke ila ndio hivyo, ni lugha ambayo sijawah isikia dunian toka nizaliwe.
Basi yule mbwa kwakweli sikumuelewa japo alikuwa akiongea, kwa lugha ile, ila nikaja kujua kumbe viumbe vyote vya humo ndani wanaongea vile, basi akatokea, mdada mmoja hivi, akawa amenisogelea, akawa ameketi, ile kuketi kwake na ule urefu wake, ikawa kama niliposimama namfikia kwenye manyonyo yake, basi na yeye akawa ametoa ishara za kuniuliza, kauliza ya kwanza, kauliza ya pili, kauliza ya tatu kwa hasira.
Ila sasa mimi sielewi basi, akawa ameniwekea mkono kichwani kwangu, hapo ndipo nikaanza kusikia kwa lugha yao, nikajibu kwa kiswahili ila nikajikuta kama sauti inayotoka ni kama ya kwao, niliulizwa hivi patwapotasa makisamaleku? Akiwa na maana kwanini unapita eneo lile ukiwa umelewa? Na ni kila siku, nikajibu kwa kikwetu, kumbe kila lugha utayoongea wewe wao wanaelewa, nilikuja gundua hili baada ya kubadili, kuongea lugha tano pale, na lengo langu nisieleweke, ili wajue sijui kinachoendelea kumbuka toka aniwekee mkono kichwan ndipo wao nilikuwa nawaelewa.