Pombe inaharibu maisha yangu nisaidieni

Halafu pombe yenyewe ukiionja ilivyo mbaya, na unaambiwa mtu anaseka nayo ni maajabu...
 
Pole sana Mkuu,
Tia nia badili starehe, badili watu.
Kama uko Single oa mke tena mwenye malezi chanya.
Elekeza pesa zako kwenye mirad ya moja kwa moja epuka kutembea na Cash au Card.
Weekend au baada ya kazi tafuta kazi zingine za kufanya kuepuka upweke.
Ukishindwa kabisa hama huo mtaa kaish na jamii isiokubaliana na tabia za aina yako au Okoka/Slim jikite kwenye mambo ya ibada.
 
kiboko ya addiction ni strong will,....wengi wenu mnajiendekeza tu,....ukiamua unaacha,.. kikubwa ni kuamua tu maisha ya ulevi au maisha ya maana,....
 
Pombe kitu kibaya sana pombe ina vinasaba vyote vya uharibifu epukana nayo,epuka marafiki vishawishi,tenga muda wa kunywa iwe weekend tu kama umeshindwa kuacha pia inabidi uoe kama hujaoa usela nao ni tatizo sana kwa sisi vijana
 
Tena upo halmashauri. Wewe umekwisha jombaa. Hao jamaa wakipata pesa ni pombe tu.
Utawasikia mkuu. Mkuu
 

Pole sana. Kutambua tatizo ni nusu ya kupata jawabu.
 
Nina shukuru Mungu niliacha kabisaa, now ni miaka kama kumi hivi inawezekana kabisa. Wewe umepoteza simu tatu! Mimi ni zaidi ya sita! Kiukweli pombe ina mateso mengi sana
 
Andika barua ya kuacha kazi.
 
Ingia YouTube mtafute mtu anaitwa David Goggins au tafuta kitabu chake kinaitwa never finished..... Acha kuendekeza mambo ya kipuuzi mzee
 
Tatizo lako ndugu yangu ni spiritual. Linatakiwa kushuhulikiwa spiritually. Pole sana..embu nitakutafuta nimewiwa tu kukusaidia...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…