Pombe ni starehe isiyofaa

Restless Hustler

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2017
Posts
5,150
Reaction score
20,025
Wenyewe husema Ukiinywa kwa taadhari kubwa haina Shida. Tatizo Ni kwamba huwezi kunywa kiasi kidogo kila siku, lazima uongeze gradually kadiri siku zinavyoenda hadi ikuharibu magoti.

Kuna fundi ujenzi nilimwomba anifanyie kazi fulani, eti akaogopa kusimama juu ya pipa kisa maungo ya mifupa hayana nguvu, chanzo ni pombe.

Kwa upande wangu naona Bora hata bangi iruhusiwe halafu pombe ipigwe marufuku kwani sijawahi kumuona mvutabangi anakosa nguvu ya Kufanya kazi au anasababisha ajali barabarani tofauti na walevi wa pombe wafanyavyo.

Hata Matatizo ya nguvu za kiume huwakumba watu Wengi wanaotumia vinywaji vikali.
 
Mkuu biashara hiyo.
serikali inapiga pesa kupitia hiyo biashara.

ngoja wanywaji waje hapa ujibishane nao akinasisi tujifunze uwenda kuna kitu kikubwa huwa tunamiss.
nawasikiaga tu wanasepa shtua upate vibe .
 
Watu wanaokunywa soda siku zote huwa ni wanafiki , Sisi hata hatuna habari nao !! Ila sasa wanavyohangaika na sisi

"Did you know 14 muscles are activated when opening a beer? Fitness is my passion.”

DJ walete 😂😂😂
 
Nakuunga mkono


( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ )

المائدة (90) Al-Maaida

Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.



( إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ )

المائدة (91) Al-Maaida

Hakika Shet'ani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha?
 
Yesu mwana wa Mungu aliona umuhimu wa pombe pale katika harusi ya Kanani, sembuse wewe binadamu. Pombe ni kinywaji kizuri kinachochangamsha akili. Kuna daktari mmoja akipiga beer mbili upasuaji anaufanya kwa weledi wa hali ya juu. Angalia wanasayansi karibu wote wanapiga kinywaji.
 
Pombe ni kinywaji cha kawaida.

Inakuwaje watu wana glorify pombe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…