[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji28]Kuna mwana akilewa ile tikatika ..utakuta anatulia kainamisha kichwa..akinyanyua kichwa juu ni kilio[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kwa wenyeji wa mbeya tukuyu, kuna siku nilikula mzinga moja na nusu wa kvant nikatoka pale saa saba usiku, ili nielekee home kwa baba angu mkubwa (bagamoyo), bs bhana mpaka kunakucha saa kumi na mbili kasoro nipo kweny michai ya kymbila naitafuta njia ya kwenda bagamoyo. Hahahaha. Nilishangaa sana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kuna jamaa langu likikolea mtindi linaanza mambo ya kisenge ,linaweza kuwaungia stori utasikia yule jamaa aliyekamatwa anampiga mashine Nguruwe Dodoma mnamjua? Wadau wakijibu hatumjui .Linanitaja mimi eti ndio huyu hapa ni rafiki yangu .Na mambo mengine ya kishenzi shenzi.
Usije ukamsikiliza mlevi atakulaza mlango wazi.Halafu mlevi akiongea kitu ni cha ukweli
Siku tumetoka na mdogo wetu mmoja wa kiume baada ya kulewa si akaanzisha jihad mule ndani anataka kutupiga mimi na bro, wakamtuliza washkaji tuliokua tumetoka nao. Baadae usiku mkali tumerudi ghetto na wale washkaji maana tuliona watapata shida ya usafiri usiku, basi nikampeleka dogo kitandani akalala na washkaji zetu wawili, washkaji wengine nikawapeleka chumba kingine wakalala na bro. Wakabaki watatu nikatoa godoro moja sebleni wakalala mimi nikalala kwenye sofa. Baadae dogo si akaamka katoka chumbani kaja sebleni kavua boxer akaanza kuwakojolea wale jamaa wamelala pale chini, jamaa mmoja ndio akaanza kumuita dogo anamwambia dogo " yani unanikojolea kweli" ila hawawezi hata kujigusa yani walikua wamelewa vibaya sana ndio mimi kushtuka ila dogo kashawaloanisha mkojo wa kutosha. Wale washakaji hua wanacheka sana wakikutana na dogo.
🤣🤣🤣🤣Huyo wa Shati kibokoKuna wana wakilewa pombe wanakua wakorofi kinoma, wanajikuta mbaaavuuu.
Kuna mmoja siku moja tulikua nae keko kanywa kaiva, akaanza kuleta mipango sio, baunsa yeye...ukimwambia atulie anakuvunjia chupa. Akakutana na vichwa vya keko kilichofuata hapo tulibaki kumuangalia tu maana alizidi ubishi.
Kuna mwingine asipolewa mpoleee...akilewa Sasa anavyocheza mziki na style zake za peke yake😂😂😂...wakati huo shati kaivua kaifunga kichwani Kama Rambo....😂😂😂😂😂
Namba moja mwamba Sana🤣🤣🤣🤣🤣🤣Mambo vipi wale vijana wote wenye maini na figo safi kabisa kwa utendaji kazi mwilini, lakini inakuaje wanangu wote wazee wa kamnyweso, wazee wa kula gambe, kula kilaji, kuuchapa mtungi na kumwagilia moyo. Dah, huko maeneo yetu (bar, clubs, vijiweni, vilabuni, mtaani) tukishaelewa tunakua na vituko na matukio mengi sana.
Haya ni baadhi ya matukio/vituko vya wanangu wakisha kula pombe (gambe).
1. Hahah kuna mwanangu mmoja siku hiyo tumekula pombe kufika mida ya nane usiku tukapoteana, kufika asubuh napigiwa simu jamaa kawekwa ndani kituo cha polisi, chap chap mpaka pale nilishangaa kuambiwa eti jamaa alienda kumchenjia askari flani pale pale kituoni usiku wa manane kisa eti askar anamfatilia demu wake, jamaa alikula kichapo mpaka alikua hawezi kutembea.
2. Kuna mwanangu yeye hata awe na millioni mfukoni, anakula bingwa au balimi tu, sasa akishakolea tu mtajuta mliekuja nae, anaenda kwenyemeza zingne na kuwaambia wadada "mmewaona wale jamaa pale (tuliokuja nae sasa) wamesema agizeni serengeti kadhaa wao watalipia.
Huyo mwanangu namba 2 akishakolea usimruhusu akatoka mezani, akitoka tu basi kuna mawili, wakaja wahudumu kukudai bill au akaja mdada akidai et umemuita.
3. Nina huyo mwanangu anakunywa pombe mara moja kwa mwezi, ila akienda tu kunywa lazma arudi home bila simu afu miguuni peku au kavaa kiatu kimoja.
Hivi inakuaje mtu anazima lakini hajikojolei kitandani?Kuna zile pigo, upo sehem unakula kilaji! Ubongo unazima ghafla, unastuka kumekucha upo kitandani, huelewi hata umefikaje