Pombe ya mnazi (palm wine) ingeweza kututoa kiuchumi

Pombe ya mnazi (palm wine) ingeweza kututoa kiuchumi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Pombe ya mnazi ni asilia, haihitaji chachu, inachachuka yenyewe. Kwa sisi watu wa Pwani hii pombe ni sehemu ya mila. Kwenye matambiko, posa au harusi ni lazima iwepo.

Hili nimeligundua hata kwa wenzetu wa Afrika Magharibi, pombe ya mnazi ndiyo anapewa binti kumkabidhi mchumba wake siku ya utambulisho. Lakini wenzetu wamejiongeza zaidi. Pombe ya mnazi wanaiuza kwenye chupa zenye mfuniko madhubuti.

Pombe hii husafirishwa, hata Wanageria wanaoishi Canada wanaweza kwenda kwenye mgahawa unaopika vyakula vyao na kuagiza pombe ya mnazi.

Tukijiongeza sokowla pombe hii haliko Pwani tu, hii ni pombe inayonywewa hata kwenye visiwa vya Fiji na sehemu nyingi walimazo na watumiazo nazi.

Ni swala la kutafuta soko na kuboresha packaging yetu. Pia kuandaa katika mazingira safi.

1550912618131.jpeg

Hivi ndivyo wenzetu wanavyo isafirisha
 
Napendelea zaidi wanzuki kuliko mnazi.mnazi ili unoge inanibidi nichanganye na choya nusu Lita hivi ndo nitafurahia
By mchemia mkuu chimbo flani
 
Palm wine drinkards oyee -bring on the tapster-manifest sir. Hivi shelf life ya mnazi muda?
 
Ukiishi na mnywaji wa mnazi unatakiwa uwe na tahadhari ya matumizi ya choo. Akikutaimu akawahi chooni utaikoma harufu ya huo mdanga.
Hahahaaah ukipishana tu na baskeli ndio imetoka kuuchukua hiyo harufu ni hatari sasa chooni mkuu c unaweza kuzima?
 
Hahahaaah ukipishana tu na baskeli ndio imetoka kuuchukua hiyo harufu ni hatari sasa chooni mkuu c unaweza kuzima?
Usiombe ukaishi nyumba ya kupanga maeneo ya Muheza! Ni balaa!! Halafu wanywaji huwa wanavitambi flani kama wanakwashakoo na wabishi sana pindi wanapoambiwa kudeki choo
 
Back
Top Bottom