Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Pombe ya mnazi ni asilia, haihitaji chachu, inachachuka yenyewe. Kwa sisi watu wa Pwani hii pombe ni sehemu ya mila. Kwenye matambiko, posa au harusi ni lazima iwepo.
Hili nimeligundua hata kwa wenzetu wa Afrika Magharibi, pombe ya mnazi ndiyo anapewa binti kumkabidhi mchumba wake siku ya utambulisho. Lakini wenzetu wamejiongeza zaidi. Pombe ya mnazi wanaiuza kwenye chupa zenye mfuniko madhubuti.
Pombe hii husafirishwa, hata Wanageria wanaoishi Canada wanaweza kwenda kwenye mgahawa unaopika vyakula vyao na kuagiza pombe ya mnazi.
Tukijiongeza sokowla pombe hii haliko Pwani tu, hii ni pombe inayonywewa hata kwenye visiwa vya Fiji na sehemu nyingi walimazo na watumiazo nazi.
Ni swala la kutafuta soko na kuboresha packaging yetu. Pia kuandaa katika mazingira safi.
Hivi ndivyo wenzetu wanavyo isafirisha