Kila mara nasisitiza Watanzania tupendane,tuheshimiane, na katu mmoja wetu asifurahie mwenzake anapopatwa na janga.Wapo wana jamvi ambao wao huweka mbele zaidi imani zao,tena kwa namna ya kuudhi imani nyingine,wakifiki kwa kufanya hivyo mama yetu Tanzania atadumu na kusimama,nao wapate nafasi ya kufanya wanayoyataka.WANAJIDANGANYA!!!Narudia,tusiposhikamana na kurudi enzi za Juma na Rosa,tunawatengenezea watoto wetu dimbwi kubwa la damu(Mwenyezi Apishie mbali)Mwislam ni lazima aheshimu matukufu ya Mkristu,na Mkristu pia ni lazima aheshimu matukufu ya Mwislam.Sisi sote ni Wana wa Ibrahim(amani iwe juu yake).Inanishangaza sana tunasahau asili yetu.Tukipendana Mwenyezi Mungu Atateremsha baraka Zake na nchi yetu itameremeta.Maadui wanajua Mwenyezi Ametupa mali asili nyingi,hali ya kua wao hawakupewa.Wamejaribu sana kutugawa wameshindwa.Sasa wanatumia dini.Sisi badala ya kushituka,bila kujijua tunashangilia.Tuamke leo maana huenda kesho ikatukuta tumechelewa.Tumsifu Yesu Kristu,Asalaam alaykum