Sumu ndiye yupi tena mkuu Mutakyamirwa ? Kwa nini inakushangaza yeye kuwa na mawazo kama yangu?
Msamehe bure ndugu yangu tumetofautiana sana japo njaa inachangia.unaota?????mbona haya uandikayo hayaendan na mjadala?
Yesu na ponda vinahusiana hapa?
LEO MAKAHAKA KUU YA KISUTU IMEMUACHIA SHEKH ISSA PONDA
KWA MADAI YAKE YA MSINGI KUHUSIANA NA KIWANJA CHA WAISLAMU CHANG'OMBE KUUZWA NA TAASISI YA BAKWATA(CCM B),ALIFUNGULIWA MASHTAKA YA UCHOCHEZI, WIZI, KUVAMIA ENEO LA WATU, NA KUTOKANA NA MASHTAKA HAYO ALINYIMWA DHAMANA KWA KIPINDI CHOTE HIKI, LEO KAACHIWA, SUALI LANGU KWA WANASHERIA HUMU,
JE, KUACHIWA KWAKE KUNAMAANISHA MADAI YAKE KWA KIWANJA CHA CHANG'OMBE NI SAHIHI?
KM NI HIVYO,JE WAISLAMU WANAWEZA KUFUNGUA MASHTAKA YA KUDAI KIWANJA CHAO KUTOKA KWA BAKWATA(taasisi ambayo CCM na serikaliyake wanaitumia kisiasa zaidi kuliko dinni,na kufanywa wanaharakati waonekane wakorofi kwa kuipinga bawkata).
JE. PONDA NAEZA KUIFUNGILIA MASHTAKA SERIKALI KWA KUMUWEKA NDANI PASINA KOSA?
Ponda hakuwekwa ndani bila kosa na ndio maana amefungwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja.
Usahihi wa madai ya Ponda haumpi haki ya kuvunja sheria nyingine. Ponda kama anayo madai dhidi ya mtu yeyote yule, anachotakiwa kufanya ni kuyapeleka madai yake mahakamani.
BAKWATA kweli ni tatizo lkn sijajua suluhisho lake. Je kuna namna ya kuwaunganisha Shiite, Sunni, Ahmaddiya, Mawahabi, Answar Sunni, Ismailliya na wengineo na kuwapa kiti kimoja?
Sawa sawa mkuu, lakini unajua kuwa katika taasisi zinazoongoza kwa rushwa nchini, mahakama ipo juu?
mods vitu kama hivi futilia mbali yataamambo yasio faa hapa
Mahakama imetenda haki na maamuzi yake yaheshimiwe.
Kila mara nasisitiza Watanzania tupendane,tuheshimiane, na katu mmoja wetu asifurahie mwenzake anapopatwa na janga.Wapo wana jamvi ambao wao huweka mbele zaidi imani zao,tena kwa namna ya kuudhi imani nyingine,wakifiki kwa kufanya hivyo mama yetu Tanzania atadumu na kusimama,nao wapate nafasi ya kufanya wanayoyataka.WANAJIDANGANYA!!!Narudia,tusiposhikamana na kurudi enzi za Juma na Rosa,tunawatengenezea watoto wetu dimbwi kubwa la damu(Mwenyezi Apishie mbali)Mwislam ni lazima aheshimu matukufu ya Mkristu,na Mkristu pia ni lazima aheshimu matukufu ya Mwislam.Sisi sote ni Wana wa Ibrahim(amani iwe juu yake).Inanishangaza sana tunasahau asili yetu.Tukipendana Mwenyezi Mungu Atateremsha baraka Zake na nchi yetu itameremeta.Maadui wanajua Mwenyezi Ametupa mali asili nyingi,hali ya kua wao hawakupewa.Wamejaribu sana kutugawa wameshindwa.Sasa wanatumia dini.Sisi badala ya kushituka,bila kujijua tunashangilia.Tuamke leo maana huenda kesho ikatukuta tumechelewa.Tumsifu Yesu Kristu,Asalaam alaykum
Hapa kuna walakini na usalama wa wahusika, kwanini wasingesubiri makovu ya Arusha yakauke miongoni mwa wakristu dio hukumu ikatoka? hali kama hii itazidisha maswali miongoni mwetu juu ya juhudi za serikali kuzika mitafaruku ya kidini. siungi hoja mkono kamwe!