Ponda alipuka-maisha ya gerezani

tunduruboy

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2013
Posts
423
Reaction score
218
*Asema mkakati wa kukamatwa kwake uliandaliwa

Sheikh Ponda Issa Ponda
SIKU moja baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dares Salaam, kumwachia na kumweka chini ya uangalizi wa mwaka mmoja Katibu Mkuuwa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda,jana aliibuka na kusema umefika wakati wa Waislamu kufanya uamuzi mzito.

Akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu, baada ya swalaya Ijumaa katika Msikiti wa Mtambani, Dar es Salaam, Sheikh Ponda, alisema hatua ya yeye kuwekwa ndani kamwe haitamkatisha tamaa na kurudi nyuma katika mapambano ya madai ya Waislamu nchini.

Alisema kutokana na hali hiyo, kwa muda mrefu Waislamu wamekuwa wakinyanyaswa kinyume cha sheria, wakati wana madai ya msingi ndani yataifa lao.

Alisema hatua yeye kukamatwa, ni wazi ilikuwa ni mkakati maalum unaoratibiwa na Serikali, wenye lengo la kuwafunga midomo masheikh waKiislamu ili wasiseme jambo lolote ambalo ni manyanyaso kwa jamii yao.

"Ni wazi hivi sasa, hawa wenzetu wanapigana nasi kitaalamu kwa kutunyamazisha midomo, kamwe hatuwezi kurudi nyuma. Hali ya Waislamu ni nzitona tunahitaji kufanya maamuzi mazito.

"Ni wazi kabisa, ninataka kulisema hili lieleweke kuwaUislamu wetu hauko kwa ajili ya Katiba, wala Utanzania wetu, bali ni kwa ajiliya asili ya dini yetu tu.

"Kwa muda mrefu, walikuwa wakifanya mikakati ya kunishughulikia eti sio raia wa Tanzania,niliwajibu wazi pale Mtoni kuwa hakuna mtu yeyote wa kuniweza kuninyang'anya.Na sasa wamebadili mfumo wa kutushughulikia masheikh kwa kesi za uongo.

"Ninataka kuwaambieni ndugu zangu, Waislamu hatutarudi nyuma, iwe katika amani au mapambano, ili mradi tu tuweze kuisongesha mbeledini ya Allah (Mwenyezi Mungu)," alisema Sheikh Ponda.


Maisha yagerezani
Alitumia mkusanyiko huo, kusimulia maisha aliyokumbana nayokatika gereza la Segerea.

Alisema aliweza kushuhudia mambo mengi, yakiwamo ya watu wengi kuwekwa mahabusu bila kesi zao kushughulikiwa.

"Walipo nikamata walinipeleka katika gereza la Segerea nakuniweka selo ya watoto, ambapo alikuja mtoto mdogo ambaye nilimuhoji na kusemaana umri wa miaka 10.

"Katika hali ya kushangaza, mtoto yule alisema amewekwa ndani kwa sababu ya tuhuma za kuiba pochi iliyokuwa na Sh 40,000.

"Kama iliwezekana kwa mtoto huyo kukamatwa, imekuwaje kwa mtoto aliye kojolea Koran pale Mbagala Oktoba 10,mwaka jana, hadi leo hajakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

"Leo hii, kwa mujibu wa takwimu zetu zinaonyesha magereza mengi na makaburi nchini yamejaa masheikh ambao kila mara wamekuwa wakifikwa namadhila ya kesi za kusingiziwa.

"Leo kina Sheikh Farid, Mselem hadi leo hii maskini ya Mungu wamewekwa ndani kwa kesi za kusingizia tu, ila Mbeya yametokea machafuko katiya Wakristo ambao walichoma msikiti, lakini hadi leo hii hakuna hata kiongozi aliyefikishwa mahakamani."

Wakati akiyasema hayo, waumini wa dini ya Kiislam kila marawalikuwa wakikubaliana na maelezo yake kwa kutamka ‘Takbir ... Takbir' neno lenye maana kwa lugha ya Kiarabu ‘Mungu mkubwa'.

Juzi Mei 9, mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimtia hatiani Sheikh Ponda na wenzake 49, ambao waliachiwa huru katika kesi iliyo kuwa ikiwakabili.

Washtakiwa hao, waliachiwa huru na Hakimu Mkazi wa Mahakamaya Hakimu Mkazi Kisutu, Victoria Nongwa.

Katika kesi hiyo, upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakiliwa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka na upande wa utetezi uliwakilishwa naWakili Yahya Njama.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Nongwa alisema: "Jamhuri imeshindwa kuthibitisha mashtaka kuanzia shtaka la kwanza, tatu, nne na la tanokwa washtakiwa wote, katika mashtaka hayo washtakiwa wote kuanzia wa kwanzahadi 50 hawana hatia.

"Katika shtaka la pili la kuingia kwa nguvu katika Uwanja waMarkaz Chang'ombe, upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha kwamba Pondaaliingia kwa nguvu, hivyo anatiwa hatiani kwa kosa hilo.

"Shtaka la kuingia kwa nguvu halielezi adhabu inayostahili kutolewa, lakini mahakama inaweza kumpa adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela au faini au vyote kwa pamoja.

"Kwa mshtakiwa wa kwanza (Ponda) hakuna kumbukumbu kwamba nimkosaji wa makosa mengine… mahakama inazingatia pia mshtakiwa alikaa rumande kwa muda mrefu kuanzia Oktoba 18 mwaka jana hadi leo, hivyo inamwachiwa kwamasharti.

Alisema mahakama inamwachia Ponda kwa masharti ya kulindaamani, awe mwenye tabia njema kwa miezi 12 na endapo atashindwa atarudi mahakamani apewe adhabu nyingine inayostahili.


SOURCE MTANZANIA
 
Ponda please what is it that you want the money u have been given by the arabs is haunting you
 
Namkumbuka Benjamin william Mkapa alisimamia amani ya nchi hakukuwepo na watu wachochezi kama huyu ponda.
 
Go go go PONDA,,,,,,
TAQBIIIIIIIIIIR,TAQBIIIIIIIIIR,TAQBIIIIIIIIR,
PONDA UMENENA NA ULILONENA LINA UKWELI,KAMA KUNA MTU ANA USHAHID WA YULE MTOTO KUWA KESI YAKE IKO MAHAKAMAN AUWEKE HAPA,,,,MSIISHIE KUMSHUTUMU PONDA BILA SABABU ZA MSINGI,
 
mi siamini kabisa kwamba serikali imeshindwa kumthibiti huyu jamaa ..........
 
Haramu ni haramu, Kweli Ponda ni janga na hana hadhi ya kuitwa shehk.

Kweli huyu mtu sio riziki kabisa.
 
Namkumbuka Benjamin william Mkapa alisimamia amani ya nchi hakukuwepo na watu wachochezi kama huyu ponda.

ila aliuza rasilimali za nchi kwa bei ya kutupa,,,na chini ya utawala wake WAISLAM WALIUAWA MWEMBE CHAI,LAKIN KWA KUWA NI WAISLAM MNAMSIFIA,,NA ZENJI JAN 2001 WAISLAM WALIONJA JOTO YA JIWE,AU WW UMEZALIWA 2005??????
 
Tuanze kumuhesabia tu,taratibu atanasa maana ndio anachotaka na kusubiria!hajui hapo nguvu kubwa sana imetumika hadi 'akaachiwa'?aendelee aone kitakachomtokea!
 
Haramu ni haramu, Kweli Ponda ni janga na hana hadhi ya kuitwa shehk.

Kweli huyu mtu sio riziki kabisa.

hiyo tuzo ya janga unampa ww,nenda segerea ukahakikishe kuna watoto au hakuna????au hadi aseme Lema kuwa gerezan kuna watoto ndo utaamini?
 
Go go go PONDA,,,,,,
TAQBIIIIIIIIIIR,TAQBIIIIIIIIIR,TAQBIIIIIIIIR,
PONDA UMENENA NA ULILONENA LINA UKWELI,KAMA KUNA MTU ANA USHAHID WA YULE MTOTO KUWA KESI YAKE IKO MAHAKAMAN AUWEKE HAPA,,,,MSIISHIE KUMSHUTUMU PONDA BILA SABABU ZA MSINGI,

Chekelea tu huyo mchochezi gaidi lakini ipo siku utajuta kwani vita havina macho.
 
ponda ni janga, pointless arguments and very childish...kumsikiliza huyu ni kupoteza muda wa kuishi
 
Tuanze kumuhesabia tu,taratibu atanasa maana ndio anachotaka na kusubiria!hajui hapo nguvu kubwa sana imetumika hadi 'akaachiwa'?aendelee aone kitakachomtokea!

acha unafki ww,nguvu gani sasa ilotumika?serikali na mahakama wameona aibu wameamua kutoa hukumu ya kishkaj ila hakua na kesi.,,,,kwani mbona mtikila alikua na kesi ya kumkashfu kikwete na hakuonekana kuwa na hatia??je naye nguvu ilitumika???msiendeshwe kwa matukio ya zima moto
 
Ponda inabidi apime kipi muhimu. Kati ya pesa anazopewa na Waarab au utanzania kwanza
 
mi siamini kabisa kwamba serikali imeshindwa kumthibiti huyu jamaa ..........

Sio kihivyo kama unavyotaka wewe iwe..kuna utaratibu wa kudeal na vichaa mkuu, anaweza akupake choo ukachekwa wewe..
 
Ndo matatizo ya kumwacha mbwa mwenye kichaa akizurura mitaani.
Nahisi mpaka askari wa wanyamapori wamtie risasi ili asije dhuru binadamu.
 
Jana niliweka uzi wa aliyoyasema ponda,modz wakaufunga,na ndugu yangu kitila mkumbo pia ulinipinga ,kwanin nimeweka pale... ,niliweka maksudi ,na nilijua magazet pia yataripoti. Nilitaka mjue na umma utambue, ule unaoitwa 'uchochezi' ni upi? Kama huu ni uchochezi, mbona dola haijachukua hatua mpaka dakika hii? Je nikweli serikali inaöngozwa kwa mfumo kristo? Kama si kweli,mbona wanaotamka hayo hawashugulikiwi 'kwa kusema uongo na kuchochea vurugu katika jamii'. ?
 
hiyo tuzo ya janga unampa ww,nenda segerea ukahakikishe kuna watoto au hakuna????au hadi aseme Lema kuwa gerezan kuna watoto ndo utaamini?

Mkuu mimi sipingani na Ponda hata kidogo ktk kutetea haki za watu mfano wafungwa wa gerezani, Lakin tatizo ni pale anapopandikiza chuki kwa watu kama vile hii nchi wakristo wote ni wajinga.

Huyu ni mpumbavu sana lakini nashangaa viongozi wetu kumchekelea huyu mtu hatari kwa usalama wa taifa.
 
Anachokitafuta Ponda atakipata si muda mrefu. Busara zilizotumika kumunusuru ili kuepusha uvunjifu wa amani na usalama wa nchi si za milele. Kwanza kwa matamushi hayo tu tayari amenza kufanya uchochezi. Nafikiri afutiwe kifungo cha nje aanze cha ndani.
 
ila aliuza rasilimali za nchi kwa bei ya kutupa,,,na chini ya utawala wake WAISLAM WALIUAWA MWEMBE CHAI,LAKIN KWA KUWA NI WAISLAM MNAMSIFIA,,NA ZENJI JAN 2001 WAISLAM WALIONJA JOTO YA JIWE,AU WW UMEZALIWA 2005??????

Pia usisahau kuwa mkapa ndiye aliyegawa majengo ya TANESCO ili kubalance mambo ya kielimu hapa nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…