Yaya makelele
Member
- Feb 3, 2013
- 40
- 5
Tuanze kumuhesabia tu,taratibu atanasa maana ndio anachotaka na kusubiria!hajui hapo nguvu kubwa sana imetumika hadi 'akaachiwa'?aendelee aone kitakachomtokea!
Usiwashangae wengine wafuata mkumbo tu haohiyo tuzo ya janga unampa ww,nenda segerea ukahakikishe kuna watoto au hakuna????au hadi aseme Lema kuwa gerezan kuna watoto ndo utaamini?
Dokta Makende usiki yaho:-Ponda inabidi apime kipi muhimu. Kati ya pesa anazopewa na Waarab au utanzania kwanza
uchochezi upi hapo?huyo mkapa si ndio kipindi chake wameuawa waislamu kama kuku?na nikipindi nchi imezalisha wakimbizi?au wewe unamaana ya amani ipi?Namkumbuka Benjamin william Mkapa alisimamia amani ya nchi hakukuwepo na watu wachochezi kama huyu ponda.
*Asema mkakati wa kukamatwa kwake uliandaliwa
Ponda alipuka - Maisha ya gerezani
Hata mwezi haujaisha mtu huyu aliyepewa kifungo cha Nje anakuja na Kauli kama hizi je huku ndiko tabia njema?.
Jeshi la Polisi wasipochukua hatua watabeba lawama-Kauli kama hizi ni hatari kwa Jamii na inafaa Ponda kuieleza mahakama ukweli wa hayo anayotamka kinyume na hapo anachochea na kuwaaminisha Waumini wa Kiisilamu mambo ambayo hayana ukweli na kusababisha chuki.
"Leo hii, kwa mujibu wa takwimu zetu zinaonyesha magereza mengi na makaburi nchini yamejaa masheikh ambao kila mara wamekuwa wakifikwa na madhila ya kesi za kusingiziwa.
"Kwa mshtakiwa wa kwanza (Ponda) hakuna kumbukumbu kwamba ni mkosaji wa makosa mengine… mahakama inazingatia pia mshtakiwa alikaa rumande kwa muda mrefu kuanzia Oktoba 18 mwaka jana hadi leo, hivyo inamwachiwa kwa masharti.
Alisema mahakama inamwachia Ponda kwa masharti ya kulinda amani, awe mwenye tabia njema kwa miezi 12 na endapo atashindwa atarudi mahakamani apewe adhabu nyingine inayostahili.
NIMEPITA MAHALA NIMEKUTANA NA MANENO YA BUSARA AMBAYO SIKUYATARAJIA KUYASIKIA KUTOKA KWA MWANADADA HUYU HAPA CHINI! BAHATI MBAYA ACCOUNT YAKE HAIKUNIPA OPTION YA KU-SHARE, KWA HIYO NIMEIKOPI KAMA ILIVYO, ILA NIMEKOSA VIONJO VYA PICHA YAKE NA ALIYOTUMIA.
NASHAURI TUMSOME KWA MAKINI.
Kutoka kwa Ashura Rashidi:
SALAMU KWA SHEIKH PONDA
Alaikum Asalam Waarahmatullahi Wabarakatuh, Kwanza kabisa kabla sijaeleza kile kilichoko moyon mwangu, Ninaomba kumsihi Allah afanye haya kwangu na wewe sheikh Ponda, indeed ayafanye haya kwa wa Tanzania wenzangu wote wenye nia njema na nchi yetu. 1, atupe kinga kwa kila hatari,
2, Baraka kwa kila jambo,
3, Jibu kwa kila maombi,
4,Tabasam kwa kila chozi,
5,Atujalie imani na subra katika maisha yetu,
Mweshimiwa Ponda ukae ukijua UZURI WA YUSUF A.S.
HAUKUMFANYA AJIVUNE
UTAJIRI WA SULEIMAN A.S.
HAKUMSAHAU MOLA WAKE
MARADHI YA AYOUB A.S.
HAYAKUMFANYA AMKUFURU MOLA WAKE
MIMI NA WEWE TUMEPEWA UHAI NA PUMZI BURE NA ALLAH,
JE TUNAFANYA NINI KUMRIDHISHA ALLAH? Je mola ametuagiza tufanye haya ambayo umekuwa uki hamasisha katika jamii iliyotulia na ku uenzi upendo wa mola wao?? Mweshimiwa Ponda unachochea vurugu katika jamii, huku ukisimamia hoja bandia ili kuhalalisha dhambi inayo kusukuma kufanya hivyo! Mimi binafsi sikufadhaishwa na ile hoja yako ya kudai mali zetu waislam zilizo uzwa pasipo sisi kushirikishwa. Lakin maelezo uliyo yatoa pale mtamban baada ya kuachiwa, yamenifanya kuto kukuamini tena, na kukuona kama mtu hatari sana kwa waislam kwani una ififisha tunu ya uislam na kuuaibisha mbele ya walimwengu, pili nimekuona kama mtu hatari unayeichukia amani na maendeleo ya watanzania wenzako.
Mheshimiwa Ponda, wakati ukidai kupambana mpaka mwisho, mimi kama muislam mwenzako ningekushauri kwanza upambane na ufaham wako ambao umepumbazwa na chuki, wivu, hasira dhidi ya wakristo. Ufaham huo umekupelekea kuto kuijua kweli katika maisha yako, hadi ukachukua hatua ya kujiundia uadui na watu wasio husika hata chembe. Kwahivo hautapata muafaka katika harakati hizo. Na wala hautakuwa huru daima, zaidi utakuwa mtumwa wa shetan, Ambaye yeye binafsi situ ni adui wa watanzania bali ni adui yako pia. Mapambano unayo hamasisha ni sawa na mgonjwa wa kipindu pindu anaye amua kutumia dose ya malaria, akiji sadikisha kwamba anaitibu kipindu pindu. Kitakacho fatia hapo ni mauti.
Muheshimiwa Ponda, chuki imeku jeuri nafsi yako hadi kupelekea kuto kupambanua mambo kwa kina hadi kuishia kuwa na hoja za kukurupuka, ambazo zina acha maswali kwa walio wengi, Ustaadhi Mukadam anamsifia Allah kwa kuwapa adhabu ya ugonjwa viongozi kazaa, hadi wengine kupata ajari, Kwake yeye Mukadam, ajari na magonjwa ni adhabu ya Mungu!! Je ajali mbali mbali ambazo zimekuwa zikitokea hapa nchini kwasababu ya uzembe wa viongozi, mfano meli zaidi ya moja zilizokuwa zikielekea visiwan hadi kuuwa wanachi wasio na hatia,
JE NAYO NI ADHABU YA MUNGU?? TUMEKUWA TUKISHUHUDIA VIFO MBALI MBALI KILA KONA YA NCHI, MAMIA YA MABASI YAMEPOTEZA MAELFU YA WATANZANIA, AJARI MBALI MBALI ZA MAJINI, JE WOTE WALIOKUFA KATIKA AJARI HIZI WALIUPINGA UISLAM?? AJARI HIZI TUMEKUWA TUKISHUHUDIA MPAKA WATOTO WACHANGA WASIO JUA KINACHO ENDELEA DUNIAN, JE NA WAO WANAUPINGA UISLAM??
Muheshimiwa Ponda unadai Serikali inawapendelea wakristo, ukidai serikali ilidai aliye kojolea quran alikuwa mtoto wakati wewe uko huko kifungon umewakuta watoto wa miaka 10, Je ni kweli wapo watoto wa miaka 10 kifungon, je hao watoto wa miaka 10 ni waislam , au ni wakristo?? Siungi mkono kabisa kitendo cha quran kukojolewa, na ningependa kabisa adhabu kali ichukuliwe kwa yeyote atakaye ihujumu quran, Lakini vile vile sipendi kabisa kitendo cha muheshimiwa Ponda kujumuisha kosa la watu fulan au kakundi fulan au mtu mmoja na ukristo kwa ujumla. Kwa mtizamo wake ponda unaosukumwa na chuki dhidi ya wakristo, unadhani yule mtoto alipewa baraka na kanisa kufanya udhalim ule! Kwahiyo ungetaka dhambi iliyotendeka mbagala isambae nchi nzima kuzaa dhambi nyingine zisizokuwa na lazima. Muheshimiwa ponda kwanini hatutaki kuiga busara za mtume katika kutatua matatizo mbali mbali yanayo tukabili? Pengine katizame kwenye hadithi za mtume, ujifunze kitu!
Muheshimiwa Ponda unadai NEKTA kuna udini, yaani waislam wanafelishwa?? Ukaongeza serikali inapendelewa na kuendeshwa na wakristo. Unayaongea haya katika kipindi hiki ambacho kila kitu kimekuwa kikiwekwa wazi kila wakati na tekinolojia. Nani anaweza kukuamini katika hili, wakati kila taasisi mbali mbali, ziwe za serikali, binafsi, tunapishana na watu wa imani tofauti? Sheikh ponda unataka kutusadikisha waislam kwamba wafanyakazi wote wa nchi hii ni wakristo, kwasababu wengi wanaofanya kazi ni wale walio elimika, unataka tuamini waislam wote nchini ni wamachinga, au wanauza nyanya na vitunguu sokoni?? Mheshimiwa Ponda ukiwa mahabusu, nchi yetu imeshuhudia kuporomoka kwa kiwango cha elimu hadi kupelekea 60% ya wanafunzi kufeli, je hiyo 60% ni waislam watupu?? Je waliofaulu ni wakristo watupu? Je huyo zitto unayemsifia alisomea wapi?? Au unataka tuamini kwamba alisomea LIBYA??
Tuna watu waliokamata sehem nyeti serikalini kama J.K Kikwete, Dr. Ghalib Bilal, Said Mwema, Mohamed Shein, Sharif Hamad, Said Othman, Je hawa viongozi wakubwa wanasali kanisa gani?? Au walibatizwa wapi?? Kwa mtizamo wako utakuwa unawaona kama wakristo?
Muheshimiwa ponda unajua kabisa necta wanasahihisha mitihan kwa mujibu wa mafundisho ya vitabu vya mitahala, karatasi yeyote itakayo toa majibu tofauti na kile kilichokusudiwa, haitakubaliwa, sasa sijui ponda unapendekeza nini?? Mfano swali likauliza ni mnyama gani mbugan mwenye shingo ndefu kuliko wote, marko akajibu ni twiga, bashiru akajibu ni sisimizi, ungetaka nectar imfaulishe bashiru kwakuwa ni muislam?? Si ndio ponda??? Je kwa mtizamo huo nchi itakuwa na vijana wenye ufanisi wa uhakika hadi kushindana kimaendeleo na mataifa mengine??
Muheshimiwa Ponda chuki binafsi imekuelemea hadi unashindwa kupanga vizuri mchoro wa dhambi yako, matokeo yake inakuumbua, eti serikali haijawahi kuwauwa wakristo?? Mara ngapi tunasikia kesi za polisi kuwauwa raia wasio na hatia, je wanao uwawa wote ni waislam? Au kwako Tanzania ni mwembechai na pemba tu?? Hivi pale anapo uwawa mkristo mbona upagusii, na wala hapa kuumi?? Inaonekana utakuwa unapinga tamko la bakwata kulaani tukio la bomu lililo lipuliwa arusha, Ila nina nshukuru mola, umeudhihirishia umma wa watanzania kwamba wewe ni mtu wa aina gani.
Ponda unalalamika kwanini wamekamatwa waarabu bali sio wazungu, unadai kamata ile ni kuwaonea waarabu na uislam? SHAMELESS SPEECH!! Inaonekana unawajua magaidi waliopanga shambulio lile! Kwahiyo unapendekeza serikali ikamate watu wasio husika, wale walio husika waachiwe huru ili hisije kuwafadhaisha waarabu na waislam! Mheshimiwa Ponda hayo unayo tusadikisha tuamini, unayaongea kwa kumaanisha au umejificha nyuma ya mgongo wa kitu fulan kwa maslahi binafsi??
HIVI MAELEZO HAYA ULIYOTOA YANAJENGA PICHA HIPI KWA WAISLAM! KAMA SIYO KUUCHAFUA UISLAM NA KUFANYA UONEKANE HAUNA THAMAN MBELE YA WATANZANIA! TUNGETARAJIA KIONGOZI KAMA WEWE UTOE MAWAZO YATAKAYO IFANYA IMANI YETU IVUTIE MBELE YA WAISLAM WENYEWE NA HATA WALE WASIO WAISLAM, NA HIVO KUTUWEKA PAMOJA KAMA WATANZANIA. ZAIDI YA KUHAMASISHA UADUI HUSIYO KUWEPO NA HIVO KULETA MIVURUGANO KATIKA JAMII.
Muheshimiwa Ponda Hakuna kitu kizuri duniani kama kuitosheleza NAFSI iwe yenye KURIDHIKA na KUSHUKURU! Lakini kuna jambo jingine zuri mpaka MTUME (SAW) aliwahi kumuusia swahaba mmoja zaidi ya mara moja, USIKASIRIKE, USIKASIRIKE, USIKASIRIKE ! Kila yule swahaba aliporudia kutaka usia kutoka kwa mtume,basi mtume alimjibu USIKASIRIKE. Kwani Hasira huzaa chuki na chuki huzaa maudhi na maudhi huzaa kisirani na kisirani huondosha nuru njema maishani, huondosha mapenzi, maelewano, utulivu, amani, n.k Azimia kutenda mema haya, na ALLAH atatia tawfiq INSHAALLAH.
Muheshimiwa ponda haujatenda jema lolote na wala hauna tawfiq za mola. Umechagua kupambana na Mola, hivo umejichovya katika mateso na hasara. Mungu hatakubali kuona una hatarisha amani ya watu wake kwa kisingizio cha kujifanya unatujali sana waislam kumbe ni hila za nyoka wa bustanin eden aliyejifanya kuwapenda sana adam na hawa hadi kuwaongopea wale tunda alilo likataza Mungu ili wafanane nae. Kumbe nia ya nyoka yule ikiwa ni kuwaangamiza milele na kuwatenga na utukufu wa Mungu.
Mheshimiwa Ponda ukumbuke alivyosema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Anayependa kukunjuliwa riziki yake na kurefushiwa umri wake basi aunge jamaa zake]. Na kuunga jamaa kuna daraja kubwa katika Uislamu.
Enyi ndugu Waislamu! Je nyinyi mmesimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu? Je mmezifuata amri zake? Je makemeo yake na makatazo mmeyaepuka? Je mmewafanyia wema jamaa zenu na mnawatembelea?
Enyi mnaotaka kheri duniani na kesho akhera ungeni jamaa zenu na kaeni nao vizuri. Enyi waumini! Je munajua faida za kuwafanyia wema jamaa zenu? Jueni ya kwamba kuna khabari njema za duniani na kesho akhera kwa wenye kuunga jamaa zao. Miongoni mwa faida hizo ni:
Faida za Kuunga Jamaa
1-Kuunga jamaa ni alama kubwa za ukamilifu wa imani.
2-Kuunga jamaa ni sababu ya kukunjuliwa mtu katika riziki.
3-Kuunga jamaa ni sababu ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu. Ponda jamaa zako ni watanzania wote walioko katika nchi yako. Sasa kama una wahujumu kwa ajili ya maslahi binafsi, unamkosea mola wako!!
GOD BLESS MY COUNTRY AND ITS PEOPLES!!! NAIPENDA SANA NCHI YANGU, NAWAPENDA SANA WATANZANIA WENZANGU!!
Usiwe mbulula wa Mawazo na mtindio wa ubongo kwa sheria za kiislamu si ruhusa kushika quran ukiwa huna udhu (ujatawaza) mwenye kosa ni Nani kati alieleta quran na kumkabidhi mtu ambae hana udhu? Na hali halisi alijua huyu si muislamu akampa kukifanyia mzaha? Au alieletewa baada ya mabishano.kwa mtindio wako huyu aliekojolea kwa Kuwa ni mkristo tu basi ana makosa. Kwa hili hakuna haki kwa uislamu hasa kwa shekh Mkubwa na mchonganishi kama ponda na wewe mbulula
Nimeshajua upungufu wako ngoja nikuache maana ukiona mtu kashikiwa akili na Ponda basi ni lazima ujihoji mara 2.
Labda me nitoe ushuhuda kidogo kwa sababu nilikuwepo siku aliyokamatwa shekh ponda na nililishuhudia tukio la kukamatwa kwake mwanzo mpaka mwisho..
Kwa kweli sikumbuki siku wala tarehe ila ilikuwa ni pale temeke katika msikiti wa tungi, kwa wanaoufahamu msikiti huu kwa huku temeke unaitwa msikiti wa harakati, kwa maana harakati nyingi za kiislam hususani za jumuiya na taasisi kwa huku temeke huwa zinaanzia hapa.
Pale msikitini pia kuna kambi ya wanafunzi wakidato cha nne na cha sita ambao wanajiandaa na mitihani so, na mimi nilikuwa ni mmoja wa wanafunzi ambao walijiunga katika kambi msikiti huo ili kujiandaa na mtihani wa kidato cha nmne mwaka jana, 2012.
Ilikuwa kama mida ya saa sita hivi kuelekea saa saba, kumbuka tayari tulikuwa katika kipindi cha mitihani ya mwisho ya kitaifa hivyo katika muda huu tulikuwa tunajisomea na kuna baadhi ambao walikuwa wameala, kambini kwetu kulikuwa na wanafunzi takribani 84. Katika muda huo kuna watu wawili ambao waliingia mule ndani msikitini kwa kasi ya ajabu, huku mmoja akipiga makelele "vijana amkeni tujitetee" "vijana amkeni tujitetee", kiukweli kwa kasi ambayo waliigia nayo na hayo makele hakuna mtu ambaye aliendelea kusoma wala kulala.
kumbe wale wawili mmoja alikuwa ni shekh ponda ambaye sura yake tulianza kuionaa akijuika nasi pale msikitini katika mida ile mibovu kama siku tatu nyuma hivi, huyu mmoja mwengine alikuwa ni dereva wa pikipiki ambaye ndo alikuwa anamuendesha shekh kutoka huko walikotoka(eneo la markaz, chang'ombe) na sasa walikuwa wanafukuzwa na polisi, baada ya wao kuingia ndani huko nje tukawa tunasikia sauti za amri "fungua geti haraka"(polisi wakimuamrisha mlinzi wa geti la msikiti ambaye alifunga geti baada ya shekh kupita na pkipiki yao)
Sasa mule ndani kukawa battle field kati ya polisi na tuliokuwepo ndani, polisi hawakuwa wanajua kama mle msikitini kuna kambi ya wanafunzi hivyo kipindi shekh anatuamsha tujitetee polisi walidhani sisi ni walinzi wa shekh.
Alisikika polisi mmoja akisema "wakileta vurugu piga risasi" mwengine "lala chini" kwa hiyo kukawa pata shika nguo kuchanika. kitu kingine kilichotuweka kwenye wakati mgumu ni kwamba polisi hawakuwa wanamtambua shekh ponda kwa sura na ukizingatia ilikuwa usiku basi hali ikawa mbaya zaidi.
Polisi walikuwa wameandamana na bwana mmoja mwenye asili ya kiarabu ambae ndo inasemekana yeye alimtambua shekh ponda na ndiye aliyekuwa akifuatilia nyendo zake tangu harakati za kule markaz zilipoanza.
Tukiwa wanafunzi wote chini ya ulinzi wa polisi na yule bwana akifanya kutupekuwa kwa sura mpaka pale walipompata mtuhumiwa wao, jamaa walimchukua katika mazingira magumu sana. Yule bwana(shekh ponda) amebobea katika michezo ya karate hivyo haikuwa rahisi sana kumkamata kama kuku wa kizungu. kwa macho yangu nilishuhudia polisi kama watatu kama si wanne wakienda chini kwa mapigo yenye ufundi wa hali ya juu, lakini mwishoni waliweza kumdhibiti na kuondoka nae.
my take: ule utaratibu wa polisi kuja kuwakamata mashekh msikitini kisha mkaingia na viatu mpaka ndani huwa mnaamsha hisia kali sana toka kwa waumini kama nilivyoshuhudia katika tukio lile.
andika uandikavyo ila Ponda amenena na aliyonena yana ukweli,,,mtamchukia Ponda kwa dini yake tu lakin ulwel utabak uleule,,,,,Lema mlimsifiiia hapa alipozungumzia kuhusu mabom ya arusha hamkumwita mchochez,lakin ponda ni mchochez,mtikila mara kadhaa anazungumza maneno ya uchochez lakin hamkuwah kusema mchochez,maaskofu walitoa tamko la uchochez lakin hamkuwaita wachochez,nchimba anatoa kauli za uchochez kuhusu kuuawa kwa padri zenj hamkusema kama mchochez akisema Ponda ndo uchochez
*Asema mkakati wa kukamatwa kwake uliandaliwa
Sheikh Ponda Issa Ponda
SIKU moja baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dares Salaam, kumwachia na kumweka chini ya uangalizi wa mwaka mmoja Katibu Mkuuwa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda,jana aliibuka na kusema umefika wakati wa Waislamu kufanya uamuzi mzito.
Akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu, baada ya swalaya Ijumaa katika Msikiti wa Mtambani, Dar es Salaam, Sheikh Ponda, alisema hatua ya yeye kuwekwa ndani kamwe haitamkatisha tamaa na kurudi nyuma katika mapambano ya madai ya Waislamu nchini.
Alisema kutokana na hali hiyo, kwa muda mrefu Waislamu wamekuwa wakinyanyaswa kinyume cha sheria, wakati wana madai ya msingi ndani yataifa lao.
Alisema hatua yeye kukamatwa, ni wazi ilikuwa ni mkakati maalum unaoratibiwa na Serikali, wenye lengo la kuwafunga midomo masheikh waKiislamu ili wasiseme jambo lolote ambalo ni manyanyaso kwa jamii yao.
Ni wazi hivi sasa, hawa wenzetu wanapigana nasi kitaalamu kwa kutunyamazisha midomo, kamwe hatuwezi kurudi nyuma. Hali ya Waislamu ni nzitona tunahitaji kufanya maamuzi mazito.
Ni wazi kabisa, ninataka kulisema hili lieleweke kuwaUislamu wetu hauko kwa ajili ya Katiba, wala Utanzania wetu, bali ni kwa ajiliya asili ya dini yetu tu.
Kwa muda mrefu, walikuwa wakifanya mikakati ya kunishughulikia eti sio raia wa Tanzania,niliwajibu wazi pale Mtoni kuwa hakuna mtu yeyote wa kuniweza kuninyanganya.Na sasa wamebadili mfumo wa kutushughulikia masheikh kwa kesi za uongo.
Ninataka kuwaambieni ndugu zangu, Waislamu hatutarudi nyuma, iwe katika amani au mapambano, ili mradi tu tuweze kuisongesha mbeledini ya Allah (Mwenyezi Mungu), alisema Sheikh Ponda.
Maisha yagerezani
Alitumia mkusanyiko huo, kusimulia maisha aliyokumbana nayokatika gereza la Segerea.
Alisema aliweza kushuhudia mambo mengi, yakiwamo ya watu wengi kuwekwa mahabusu bila kesi zao kushughulikiwa.
Walipo nikamata walinipeleka katika gereza la Segerea nakuniweka selo ya watoto, ambapo alikuja mtoto mdogo ambaye nilimuhoji na kusemaana umri wa miaka 10.
Katika hali ya kushangaza, mtoto yule alisema amewekwa ndani kwa sababu ya tuhuma za kuiba pochi iliyokuwa na Sh 40,000.
Kama iliwezekana kwa mtoto huyo kukamatwa, imekuwaje kwa mtoto aliye kojolea Koran pale Mbagala Oktoba 10,mwaka jana, hadi leo hajakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Leo hii, kwa mujibu wa takwimu zetu zinaonyesha magereza mengi na makaburi nchini yamejaa masheikh ambao kila mara wamekuwa wakifikwa namadhila ya kesi za kusingiziwa.
Leo kina Sheikh Farid, Mselem hadi leo hii maskini ya Mungu wamewekwa ndani kwa kesi za kusingizia tu, ila Mbeya yametokea machafuko katiya Wakristo ambao walichoma msikiti, lakini hadi leo hii hakuna hata kiongozi aliyefikishwa mahakamani.
Wakati akiyasema hayo, waumini wa dini ya Kiislam kila marawalikuwa wakikubaliana na maelezo yake kwa kutamka Takbir ... Takbir neno lenye maana kwa lugha ya Kiarabu Mungu mkubwa.
Juzi Mei 9, mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimtia hatiani Sheikh Ponda na wenzake 49, ambao waliachiwa huru katika kesi iliyo kuwa ikiwakabili.
Washtakiwa hao, waliachiwa huru na Hakimu Mkazi wa Mahakamaya Hakimu Mkazi Kisutu, Victoria Nongwa.
Katika kesi hiyo, upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakiliwa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka na upande wa utetezi uliwakilishwa naWakili Yahya Njama.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Nongwa alisema: Jamhuri imeshindwa kuthibitisha mashtaka kuanzia shtaka la kwanza, tatu, nne na la tanokwa washtakiwa wote, katika mashtaka hayo washtakiwa wote kuanzia wa kwanzahadi 50 hawana hatia.
Katika shtaka la pili la kuingia kwa nguvu katika Uwanja waMarkaz Changombe, upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha kwamba Pondaaliingia kwa nguvu, hivyo anatiwa hatiani kwa kosa hilo.
Shtaka la kuingia kwa nguvu halielezi adhabu inayostahili kutolewa, lakini mahakama inaweza kumpa adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela au faini au vyote kwa pamoja.
Kwa mshtakiwa wa kwanza (Ponda) hakuna kumbukumbu kwamba nimkosaji wa makosa mengine mahakama inazingatia pia mshtakiwa alikaa rumande kwa muda mrefu kuanzia Oktoba 18 mwaka jana hadi leo, hivyo inamwachiwa kwamasharti.
Alisema mahakama inamwachia Ponda kwa masharti ya kulindaamani, awe mwenye tabia njema kwa miezi 12 na endapo atashindwa atarudi mahakamani apewe adhabu nyingine inayostahili.
SOURCE MTANZANIA