Ponda hajapewa dhamama sababu mkurugenzi wa mashtaka ya jinai (DPP) amefaili certificate kuwa asipewe dhamana hiyo ni kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Mashtaka ya jinai ambapo kuna kifungu kinampa DPP mamlaka hayo hata kama kosa husika linastahili dhamana na sababu hapa zinaweza kuwa za kiusalama,maslahi ya umma n.k.
Huyo Lipumba nae hata hajui anachokiongea,moja kati ya mashtaka ya Ponda ni Criminal Tresspass, hii maana yake ni kuingia kwa jinai kwenye ardhi ya mtu mwingine,kosa hilo haliwezi kwenda mahakama ya ardhi kwani haina mamlaka ya kusikiliza kesi za jinai, hapo ilipo ndio mahala pake mkuu na Segerea ndio makazi ya yeyote anayekataa kutii sheria za nchi.