kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Niimefurahi kujiuzulu Kinana nafasi yake ndani ya chama ili kutunza heshima yake. Kwa nini nimefurahi kwa sababu ni mtu namfahamu tangu tuko vijana shule. Ni mtu mwema na rafiki kwa kila mtu na nisingependa kuona heshima yako ikipotea.
Lazima tukubali ndani ya ccm tuko wanachama wa milango tofauti kisiasa siku hizi. Wakati itikadi ya chama bado ni ile ya ujamaa na kujitegemea ikiwa na yale marekebisho enzi za mzee Ngombale Mwiru kwamba sasa tujenge ujamaa kwa kutumia sekta binafsi bado tumetofautiana wanachama jinsi gani sekta binafsi itumike ili kuinua uchumi wa umma wa wananchi.
Wengi wa vigogo wamejigeuza wao kua sekta binafsi moja kwa moja au kutumika na sekta binafsi kuendeleza maslahi yao binafsi na kusababisha malengo ya kuletea maendeleo kwa umma wa wananchi kutotekelezeka.
Ile clip mkimpiga mkwara Magufuli aliyejizolea sifa kubwa kwa wananchi wanyonge na wapenda maendeleo kote nchini na nje ya nchi hakika haikuwaacha salama. Wengi wa wanaccm wamepoteza imani na nyie mliyosikika kifichoni mkimkejeli na kumdharau Magufuli.
Hata bada ya kumuomba msamaha wenzako Nape na Januari baada ya kurejeshwa uongozini wamekua wanampiga vijembe kupinga umagufuli jambo ambalo limewaletea kuchukiwa.
PIA SOMA
- News Alert: - Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia