Pongezi kituo cha afya GAIRO

lufungulo k

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2012
Posts
2,601
Reaction score
2,058
Napenda kutoa pongezi za dhati kwa Serikali na kituo cha afya GAIRO, nimekwenda kupata HUDUMA majira ya saa 14:00.

Nimepokelewa vzr, toka mapokezi mpaka kwa daktari. Baada ya maelezo kwanza nimepimwa pressure.

Kisha nikaelekezwa niende MAABARA. nimechukuliwa vipimo. Jamani hili kipindi cha nyuma HALIKUWEPO uende mchana !!! Kwenye Zahanati ya UMMA!! upate vipimo!! yaani ningeambiwa njoo kesho kwa vipimo au nenda pale nje kwenye vipimo binafsi.

Nimepimwa na kupata dawa . Ahsanteni kwa HUDUMA BORA. HONGERENI pia kwa USAFI wa malengo yenu.

Choo safi.
 
Mganga mfawidhi anajipa promo🤣🤣🤣


Nishukuru ni mimi ndio nimekupima izo VITAL SIGNS
 
Una uhakika wewe sio muhudumu hapo hospitali?
 
Labda ulienda na gari, si unatujua wabongo na ndinga
 
Una uhakika wewe sio muhudumu hapo hospitali?
Mhhh, tujenge tabia ya kuaminiana. Ndo mara yangu ya 1 kufika eneo lile.

Mm ni mkazi wa Dar es Salaam. Nimepata huduma na jicho langu la kiuchunguzi. WABONGO hatujipendi hasa MAENEO ya vyoo.

Lkn pale nimekuta choo safi na sakafu iko safi kwenye majengo mengine kwakweli nimefarijika mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…