Leo kwenye pitapita zangu youtube ghafla nikakutana na huu wimbo unaitwa Tunafanana kaimba msanii Barnaba kusema kweli toka uvunguni wa moyo wangu wimbo huu ni mzuri sana kimashairi na melody Barnaba kautendea haki na ukija upande wa beat Deey Classic nae amewakilisha vizuri.
Video imefanywa na Travellah nae hajamuangusha kwani graphics, rangi, location na hata video queen amefit kwenye video
Huu jamaa ana kipaji sana japo wabongo wanamchukulia simple angekuwa kwa wenzetu angekuwa mbali sana
N.B mie sio Barnaba na wala sijatumwa na nae kuja kumpa promo ni mtizamo wangu tu.